Wajumbe wa kamati ya lishe Halmashauri ya wilaya Kalambo mkoani Rukwa wameazimia fedha za utekezaji wa afua za lishe kwa mwaka wa fedha 2025/2026 kuelezwa katika utekelezaji wa afua za lishe vijijini ikiwemo utoaji elimu kwa wanawake wajawazito na wananchi.
Awali akiongea kupitia kikao hicho Afisa Lishe wa Halmashauri Ndugu Robert Tepeli kupitia kikao cha maandalizi ya bajeti ya lishe kwa mwaka wa fedha 2025/2026, amesema lengo la serikali ni kutokomeza utapia mlo na udumavu kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndugu Wambura Sunday amesema katika Mwaka wa fedha 2025/2026 halmashauri imejipanga kuongeza kasi ya utoaji wa elimu vijijini kwa kushirikiana na viongozi wa serikali za vijiji, watendaji na viongozi wa dini kupitia maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji na maadhimisho ya siku ya afya na lishe ambayo hufanyika kila robo na kwamba yatafanyika kwa kila kata.
Hata hivyo utekelezaji wa mkataba wa lishe unaenda sambamba na matumizi ya fedha zilizotengwa katika mpango kazi wa mwaka husika kiasi cha shjilingi 1000/= ambapo kwa mwaka wa fedha 2024/2025 Halmashauri ilitenga jumla ya fedha 81,614,676.630020/=
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.