Wajumbe saba wakazi wa kijiji cha Singiwe wilaya ya Kalambo akiwemo mtia nia ubunge wa viti maalumu Patrick Dyamukama wanashikiliwa na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU mkoani Rukwa baada ya kukamatwa wakati wakigawa fedha kiasi cha shilingi milioni nne kwa wajumbe wa UWT wilayani Kalambo.
Wajumbe hao walikamatwa katika makazi ya Yusta Kajema mkazi wa singiwe kata ya Lyowa wilayani humo wakati wakigawana fedha kiasi cha shilingi million nne (4,000,000),fedha ambazo zilikuwa zimehifadhiwa kwenye begi.
Hata hivyo katika tukio hilo maafisa TAKUKURU kutoka wilayani Kalambo walifika na kuwakuta wajumbe hao wakijaribu kugawana fedha ambazo zilikuwa zimehifadhiwa kwenye bahasha 20 huku kila moja ikiwa na kiasi cha shilingi laki mbili.
Kufuatia hali hiyoTaasisi hiyo iliwakamata wajumbe hao kwa mahojiano na kukili kupewa fedha hizo na Patrick Ndyamukama kama kishawishi cha kumpigia kura tarehe 23/7/2020 kwenye uchaguzi.
Mkuu wa TAKUKURU mkoani Rukwa Hamza Mwenda, alisema ‘’baada ya kupata taarifa hiyo maafisa wa TAKUKURU wilayani kalambo waliweza kufika katika kijiji cha Singiwe na kufanikiwa kuwaweka chini ya ulinzi wajumbe 7 wa UWT waliokuwa wamekutwa nyumbani kwa Yusta Kajema majira ya 2:46 asubuhi na baada ya kufanya upekuzi ndani ya nyumba hiyo walimkamata Irene Ndyamukama akiwa na begi lenye fedha kiasi cha shilingi million nne.’’Alisema Mwenda.
Alisema katika mahojiano yaliofanyika Irene Ndyamukama alikiri kugawa bahasha 30 kwa wajumbe therathini ambao alikutana nao asubuhi ya tarehe 21/7/2020 na kwamba alibakiwa na bahasha kumi na tisa19 kwa ajili ya wajumbe ambao walikuwa bado hawajafika eneo la tukio.
Mkuu wa TAKUKURU mkoani Rukwa Hamza Mwenda, alisema baada ya kupata taarifa kuwa Irene Ndyamukama mtia nia wa ubunge kukusudia kugawa fedha kwa wajumbe wa umoja wa wanawake (UWT) CCM wilayani Kalambo ambao ni wapiga kura za maoni kwa wagombea wa nafasi ya ubunge vitimaalumu
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.