Wakazi wa kijiji cha Namlangwa kata ya Lyowa wilayani Kalambo mkoani Rukwa wameiomba serikali kuwapatia elimu zaidi juu ya ujenzi wa nyumba imara na zenye ubora kutokana na maeneo hayo kukubwa na adha ya nyumba zao kuanguka kila mwaka kutokana na mvua kubwa ambayo imekuwa ikiambatana na upepo mkali kunyesha kisha kuharibu makazi yao na kuwasabishia hasara kubwa
Wakiongea kwa nyakati tofauti mara baada ya nyumba zao zipatazo 16 kuanguka kutokana na mvua kubwa iliokuwa imeambatana na upepo mkali kunyesha katika maeneo hayo,wamesema serikali haina budi kuingilia kati swala hilo kwa kuwapatia elimu juu ya namna ya ujezi wa nyumba bora .
Wamesema kila mwaka nyumba zimekuwa zikianguka katika maeneo hayo kutokana na kujenga nyumba kwa kutumia tope huku wengi wao wakijenga bila kuweka lenta na kusababisha kuanguka kila ifikapo wakati wa masika.
Mkuu wa wilaya hiyo Calorus Misungwi amekili kutokea tukio hilo na kuwataka wananchi kujenga nyumba zenye ubora ikiwa ni pamoja na kupanda miti kuzunguka maeneo hayo kwa lengo la kuondokana na kadhia hiyo
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.