• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Kalambo District Council
Kalambo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya sekondari
      • Maji
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo na Ushirika
      • Ufugaji na Uvuvi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Mazingira
      • TEHAMA na Uhusiano
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
      • Kituo Cha Afya Matai
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Upimaji wa Viwanja na Mipango Miji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Uongozi na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Ujenzi Uchumi na mazingira
      • UKIMWI
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Mradi unaoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Bajeti ya Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
  • Salary Slip

Wakazi Wa Kipwa Waanza Kutekeleza Agizo La Serikali Kuhamia Maeneo Ya Miinuko.'

Posted on: May 24th, 2021

Wakazi wa kijiji cha Kipwa kilichopo mpakani kati ya nchi ya Tanzania na Zambia wameanza kutekeleza agizo la Serikali la kuwataka kuhamia maeneo ya miinuko ndani ya siku 90

Kijiji cha kipwa kinapatikana kata ya Kasanga wilaya ya Kalambo kando ya ziwa Tanganyika, kutokana na jiografia hiyo kimekuwa kikikabiriwa na ongezeko la maji ya ziwa Tanganyika.

 Hata hivyo mwanzoni mwa mwaka 2021 kijiji hicho kilikumbwa na mafuriko ya maji yaliyokuwa yamesababishwa na kufurika kwa ziwa Tanganyika na kusababisha kaya 209 kukosa makazi na huku baadhi ya wananchi wakilazimika kuishi kwa majirani na sehemu za ibada huku Taasisi za Serikali zikikumbwa na kadhia hiyo.

Licha ya hilo mnamo tarehe 30 Aprili 2021 kamati ya wataalamu wa maafa kutoka Halmashauri ya Kalambo ikiongozwa na kaimu mkurugenzi Ndg. Jabiri Ally ilifika kijijini hapo kwa dhumuni la kujionea adha hiyo na kubaini asilimia 70 ya wakazi wa kijiji hicho kupatwa na adha hiyo,

Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Jabiri Ally, alisema nyumba nyingi zikiwemo za watumishi, zahanati na shule ya msingi nazo zimezungukwa na maji na kuathiri utoaji huduma za afya na elimu

“pia hali ya vyoo kwa sasa sio nzuri jambo ambalo lina hatarisha kutokea kwa janga jingine la mlipuko wa magonjwa kama kipindupindu na uti wa mgongo’’. alisema Jabiri

Hata hivyo kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo ikiongozwa na mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Kalorius Misungwi ilitembelea kijiji hicho na kuamuru  wananchi wote kuhamia maeneo ya miinuko ndani ya miezi mitatu agizo ambalo lilipokelewa kwa shangwe kubwa na  wakazi wa kijiji hicho.

Kamati hiyo pia ilitembelea maeneo ya makazi mapya ya wakazi wa kjiji hicho pamoja na maeneo ya kujenga taasisi za Serikali ikiwemo shule na zahanati.

Awali akiongea na wakazi wa kijiji hicho mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo Mhe. Kalorius Misungwi, alisema kijiji hicho kina jumla ya kaya 357 na kaya 209 zimekosa makazi na kaya 144 ndizo zilizo salia kwa hivi sasa.

Hata hivyo miongoni mwa changamoto kubwa inayowakabiri wakazi wa kijiji hicho katika maeneo mapya ya makazi wanayotarajia kuhamia ni ukosefu wa huduma ya maji pamoja na barabara.

Ziwa Tanganyika lina urefu wa km 673 na upana wa km72 huku eneo lote likiwa na km2 32,900 na ujazo wa km3 18,800 huku urefu wa ufukwe ikiwa ni km 1,828.

 Ziwa Tanganyika limezungukwa na nchi ya Tanzania, Congo, Burundi na Zambia huku wananchi kutoka sehemu zote za nchi hizo wakilitegemea katika shughuli za uvuvi na usafiri.

licha ya uwepo wa ziwa hilo lakini bado kumekuwa na changamoto ya mabadiliko ya tabia ya nchi, ambapo kwa mwaka 2020 /2021 kumekuwa na ongezeko la kupwa na kujaa kwa ziwa hilo hali ambayo imekuwa ikiwasababishia hasara wananchi na Serikali kwa ujumla.

March 30 /2021 kulitokea mabadiliko ya tabia ya nchi ambapo ziwa hilo lilijaa na kufunika kijiji na eneo lenye miundombinu muhimu ya huduma kwa umma. Miongoni mwa miondombinu iliyokumbwa na janga hilo ni viwanda, masoko na makazi ya wananchi likiwemo soko la samaki la Kasanga.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI October 03, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI September 10, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2023 July 13, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 01, 2023
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • KAMATI YA USHAURI YA MKOA WA RUKWA YARIDHIA MAPENDEKEZO YA KULIGAWA JIMBO LA KWELA.

    March 15, 2025
  • RC RUKWA AWAONYA VIONGOZI WANAOKWAMISHA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI SAMAZI

    March 14, 2025
  • WANAWAKE KALAMBO WAFANYA UTALI WA NDANI

    March 10, 2025
  • TALGWU YATOA MSAADA WA KIBINADAMU KWA WANAWAKE WANAOJIFUNGUA

    March 10, 2025
  • Tazama Zaidi

Video

MHE. RAIS SAMIA S. HASSAN AMUAPISHA MAKAMO WA RAIS MTEULE DKT. PHILIP ISDOR MPANGO IKULU CHAMWINO
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Huduma za Afya
  • Ardhi na mipango Miji
  • Kujua Kodi ya Ardhi
  • Kalambodc blog
  • TEHAMA
  • Kalmbodc Twitter
  • Kalambodc Facebook
  • Kalmbodc Instagram
  • TAMISEMI

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Wakala wa Manunuzi Serikalini
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
  • Mkoa wa Rukwa
  • Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga
  • Manispaa ya Sumbawanga

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Watu waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Matai, Kalambo, Rukwa

    Anuani ya posta: P.o box 03

    Simu ya Mezani: 025-2955212

    Simu ya mkononi: +255 622 858 482

    Email: ded@kalambodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya tovuti
    • Huduma

Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.