Serikali mkoani Rukwa kwa kushirikiana na taasisi ya utafiti wa wa kilimo {TARI} na mashirika mengine nchini, imezindua mpango mkakati wa upimaji tathimini ya udongo mradi unaotarajiwa kuwafikia wakulima wapatao 4000 katika vijji 400 kupitia wilaya tatu za mkoa huo kabla ya mwaka 2021 kuisha.
Mradi huo ni mwendelezo wa awamu ya kwanza iliyozinduliwa mwaka 2019 na kuwafikia wakulima na wadau wa kilimo wapatao 20,000 katika mikoa miwili ya Njombe na Songwe.
Awali akiongea wakati wa uzinduzi wa mradi huo, kaimu mkuu wa mkoa wa Rukwa Kalorius Misungwi,alisema mradi huo unatarajiwa kuhudumia wakulima 4000 katika vijiji 400 .
Alisema kupitia mradi huo wakulima wataweza kuinua vipato vyao kwa kulima kilimo chenye tija, na kupitia mradi huo mazao ya wakulima yataongezeka maradufu.
Mkurugezi mtendaji wa kampuni ya OCP Tanzania Dkt Mshindo Msolla, alisema kampuni yake inashirikina na Serikali kuandaa mchakato wa upimaji wa udongo kwa zaidi ya vijiji 100 ndani ya mkoa wa Rukwa
Alisema lengo kubwa ni kuwaelimisha wakulima juu ya udongo wa eneo lao bila gharama zozote, na kusisitiza kuwa majibu yatatolewa kwa wakulimu muda mfupi baada ya vipimo kufanyika.
‘’mradi huu wa upimaji udongo unatarajiwa kuendeshwa katika vijiji 400 na kuwafikia wakulima wapatao 4000 kufikia mwisho wa mwaka 2021. Mradi huo pia unatarajiwa kutoa mapendekezo ya mbolea kwa wakulima wapatao 14000 watakao wakilisha wakulima wenzao kutoka mashamba mbalimbali, kwa kutumia njia rahisi za upimaji udongo ili kupata matokeo sahihi.’’ Alisema Msolla.
Mradi wa upimaji tathimini unaoratibiwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania kupitia Wizara ya kilimo , pamoja na Taasisi ya utafiti wa kilimo TARI.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.