Wakulima wilayani Kalambo Mkoani Rukwa wametakiwa kutumia mbolea ili kuongeza tija ya uzalishaji wa mazao ya nafaka shambani kwa kuongeza bidii katika upimaji wa afya ya udongo.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi msaidizi Idara ya maendeleo na kilimo kutoka wizara ya kilimo Ndugu Samsoni Ponela wakati akiongea na wakulima katika Kata ya Matai na Mkowe wilayani Kalambo kupitia mkutano wa hadhara uliokuwa na lengo la kutoa elimu kwa wakulima juu ya matumizi sahihi ya Mbolea na kusema lengo la serikali ni kuwawezesha wakulima kunufaika na kilimo kwa kulima kwa tija.
Aidha ametumia fursa hiyo kuwataka wakulima kuachana na kilimo cha mazoea na badara yake kujikita zaidi katika kilimo chenye tija ikiwemo kufuata taratibu na kanuni zinazotolewa na wataalamu wa kilimo.
Kwa upande wake kaimu Mkurugenzi mtedaji Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Ndugu Nicholaus Mlango, amesema kwa sasa wanaendelea kuwasajili wakulima kwenye mfumo ili kupata mbolea ya RUZUKU kabla yakuanza msimu mpya wa kilimo
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.