Baada ya kilio cha muda mrefu cha wakulima katika mikoa ya Rukwa na Katavi kutolipwa fedha zao na kusababisha kuishi mazingira magumu,hatimaye serikali imetoa shilingi Bilioni 47 kwajili ya kulipa madeni ya wakulima hao.
Akiongea na wakulima katika maeneo tofauti ya mkoa wa Rukwa
Naibu waziri wa kilimo Omari Mgumba amesema yote hayo yamefanyika kutokana na serikali ya awamu ya tano kuwajali wakulima wadogo ndiyo maana imewalipa fedha kwa ajili ya mahindi hayo.
Mwenyekiti wa Mpui Saccos,Hezron Mwakajoka wakati akisoma risala ya Saccos hiyo ameiomba serikali kuitafutia saccos hiyo soko kwaajili ya mahindi yao kwani ilikopa fedha katika mabenki na kununua tani 800 ya mahindi kwania ya kuuza nchi ya Rwanda.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.