Serikali ya mkoa wa Rukwa kwa kushirikia na Kampuni ya Agricom Africa Limited imeanza hamasa kwa wakulima ili waanze kutumia zana za kisasa katika kilimo kwa kuanzia wametoa mkopo wa matrekta kwa wakulima 10 ili kuwongeza uzalishaji na kuinua kipato chao.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa kampuni ya Agricom Philipo Kulaya amesema kuwa kampuni hiyo ilianza kwa kutoa mafunzo kwa wakulima waliokidhi vigezo vya kupewa mkopo huo juu ya umuhimu wa kutumia zana za kisasa na kuachana na zana za asili.
Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Ocran Chengula amesema matumizi ya zana za kisasa za kilimo yataongeza uchumi wa wakulima hali itakayopelekea kuongeza uchumi wa taifa na kuwa na chakula cha kutosha.
Kwa upande wake Mgeni Rasmi katika hafla hiyo fupi ya makabidhiano ya matreka hayo kwa wakulima Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule ameshauri Kampuni ya Agricom Africa Limited kuweza kuwa na vipuri karibu ili wakulima watakapopatwa na shida ya uharibifu wa matrekta hayo basi iwe rahisi kutengenezwa.
Kati ya Vyama vya wakulima 166 vilivyoomba kupatiwa mkopo katika halmashauri nne za mkoa wa Rukwa ni vyama 88 tu ndivyo vilivyopita kwenye mchujo wa kupatiwa mkopo wa trekta na hivyo ndivyo pekee vitakavypatiwa mkopo huo kwa fedha taslimu na kwa mkopo.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.