• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Kalambo District Council
Kalambo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya sekondari
      • Maji
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo na Ushirika
      • Ufugaji na Uvuvi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Mazingira
      • TEHAMA na Uhusiano
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
      • Kituo Cha Afya Matai
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Upimaji wa Viwanja na Mipango Miji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Uongozi na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Ujenzi Uchumi na mazingira
      • UKIMWI
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Mradi unaoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Bajeti ya Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
  • Salary Slip

Walimu Rukwa Wapania Kubadili Tabia Za Wanafunzi Kuhusu Hedhi Shulen.

Posted on: September 2nd, 2020

Umoja wa waalimu wa Hedhi Salama kwa shule za msingi wilayani kalambo mkoani Rukwa wamepania kuhakikisha wanapunguza fikra potofu kuhusu suala la hedhi kwa wasichana wanaovunja ungo pamoja na kukomesha utoro kwa wananfunzi wa kike wanaoona aibu kuhudhuria shule pindi wanapopata hedhi kwa kutoa elimu sahihi ya suala la hedhi mashuleni.

Azma hiyo imekuja baada ya waalimu kutoka Halmashauri zote za mkoa wa Rukwa kupewa mafunzo yanayohusu namna ya kutengeneza pedi kwa kutumia aina mbalimbali za vitambaa pamoja na kukabiliana na wanafunzi wanaoona aibu ama fedheha pindi wanapopata hedhi wakiwa shuleni na hivyo kuwarahisishia Maisha yao wanapokuwa shuleni huku wakiwahamasisha kuendelea kuhudhuria shuleni ili wasiachwe nyuma kimasomo.

Aida Mwanauta ni mwalimu wa Hedhi Salama kutoka Shule ya Msingi Ilambila, Wilayani Kalambo, aliishukuru serikali kwa kuwapatia mafunzo hayo muhimu kwani changamoto wanazokumbana nazo ni nyingi na mafunzo hayo yamamsaidia kujua namna ya kuwasaidia wasichana hao pindi wanapokuwa katika hedhi kutokana na wanafunzi wengi kutokuwa na ufahamu wa kutosha juu ya namna ya kukabilina na hali hiyo.“Kuna mwanafunzi anakuja shuleni hajui ni namna gani anaweza akajistiri, mwingine anatoka nje anakimbia,huko nje anachukua hata makaratasi,majani kwaajili ya kujistiri ambayo inaweza ikamletea matatizo baadaye,kwahiyo katika semina hii tumejifunza mambo mbalimbali, tumejua ni mambo gani ambayo unaweza ukamfundisha mtoto, akajua jinsi ya kujihifadhi akiwa shuleni na hatimae akawa anasoma na asiwe mtoro shuleni,na kujiona ni sawa na wengine,” Alisema.

Nae, Mwalimu Victoria Tanganyika alisema kuwa mafunzo hayo yamemsaidia kujua vifaa vinavyotumika kutengeneza pedi za kike na namna ya kuvitekeza pamoja na kujua mazungumzo anayotakiwa kufanya na matoto ili kumshawishi aweze kujiamini na kushiriki katika michezo na masomo katika mazingira ya shule.

Kwa upande wake Mwalimu Clifonsia Remidio ameiomba serikali kuendelea kutumia njia mbalimbali za vipeperushi na kutoa semina kwa waalimu wengi zaidi wanaotoa huduma ya hedhi salama mashuleni ili kuweza kuwasaidia wanafunzi wa kike ambao wamekuwa wakipata tabu kusoma wanapokuwa katika kipindi cha hedhi.

“kuna vitu vingi tulikuwa hatuvifahamu, kuna wakati mwingine hata kama mimi mwalimu nimeshasoma lakini bado nitaona aibu kuenenda kumuelekeza yule mwanafunzi, lakini ameshatuelekeza mwezeshaji tumepata mwanga mzuri pia nimefurahi kwasababu hili suala linashirikisha pande zote mbili, upande wa waalimu wa kiume na upande wa waalimu wa kike pia kwamba tuwasaidie Watoto wanaposikia ile hali ya mabadiliko ya mwili,”Alisema.

Aidha, Mwezeshaji wa mafunzo hayo ya Hedhi Salama, Mwalimu Jesca Lwiza alisema kuwa mafunzo hayo yanalenga kutoa elimu ya hedhi salama kwa wanafunzi ili kupunguza utoro mashuleni na kuongeza kuwa wanategemea kuona mabadiliko makubwa ya mahudhurio shule kwa shule ambazo waalimu wake wamehudhuria mafunzo hayo.

“Kuna ukimya ambao upo katika masuala ya hedhi salama, wanafunzi wanakosa elimu sahihi, lakini pia wanakosa namna ya kujiamini wanapokuwa katika masomo na wakati mwingine shuleni hakuna vyumba maalum vya kujihifadhi wanapokuwa katika hedhi, kwa kulitambua hilo tumeona serikali namna ilivyoweza kuwezesha kwa kuwapa mafunzo waalimu lakini imeweza kuboresha miundombinu iliyopo mashuleni kwa kuweka vyumba hivyo,” Alisema.

Wakati akifungua mafunzo hayo Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Winnie Kijazi alisisitiza kuwa tafiti zilizofanyika zimeonesha kuwa wasichana wengi hawana taarifa za awali kuhusu hedhi za pia walipata hedhi ya kwanza pasipo kuwa na uelewa wa kutosha kuhusu mabadiliko ya miili yao hivyo mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo waalimu kufikisha elimu katika shule.

“Tafiti zinaonesha kuwa bado kuna fikra zisizo sahihi kuhusu masuala ya hedhi hususani miiko na unyanyapaa inayosababisha wasichana na wanawake kushindwa kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo na kijamii na wanafunzi wa kike kukosa baadhi ya siku za masomo na wengine kuacha shule wanapokuwa kwenye hedhi. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kulitambua hilo imeweka jitihada kuhakikisha kuwa fursa za elimu zinapatikana kwa makundi yote,” Alieleza.

Halikadhalika mratibu wa mradi wa School Water Sanitation and Hygiene (SWASH) Mwalimu Matinda Mwinuka aliwaasa waalimu kuhakikisha shule zinakuwa na vyombo maalum kwaajili ya walemavu pamoja na vyumba kwaajili ya wasichana kubadili pedi za hedhi pindi wanapokuwa katika hali hiyo nasio kutumia vyoo vya kawaida ambavyo havina mazingira mazuri ya kubadilishia vifaa vyao.

“Kuna shule moja fundi kaweka shule maalum, anasema kuwa kile ndio chumba maalum, walemavu wataingia humo humo, hedhi salama wataingia humo humo, ametoboa tundu na kuweka ‘pipe’ anasema Watoto wa kike wakishaingia humu ndimo watatumbukiza vile vitu vyao yaani ni vitu vya ajabu kwakweli.”

Mradi huo unatekelezwa katika halmashauri tatu za Mkoa wa Rukwa kwa muda wa miaka minne huku kwa mwaka wa fedha 2019/2020 Mkoa ulipewa kiasi cha Shilingi 578,486,955.63/= kwaajili ya utekelezaji wa mradi huo unaofadhiliwa na Benki ya Dunia na kutekelezwa katika mikoa 17 na Halmashauri 86 za Tanzania Bara ukiwa na lengo la kuboresha mazingira ya kufundishia, kujenga vyoo bora shuleni na kuweka miundombinu ya maji safi na salama.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI October 03, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI September 10, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2023 July 13, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 01, 2023
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • KAMATI YA USHAURI YA MKOA WA RUKWA YARIDHIA MAPENDEKEZO YA KULIGAWA JIMBO LA KWELA.

    March 15, 2025
  • RC RUKWA AWAONYA VIONGOZI WANAOKWAMISHA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI SAMAZI

    March 14, 2025
  • WANAWAKE KALAMBO WAFANYA UTALI WA NDANI

    March 10, 2025
  • TALGWU YATOA MSAADA WA KIBINADAMU KWA WANAWAKE WANAOJIFUNGUA

    March 10, 2025
  • Tazama Zaidi

Video

MHE. RAIS SAMIA S. HASSAN AMUAPISHA MAKAMO WA RAIS MTEULE DKT. PHILIP ISDOR MPANGO IKULU CHAMWINO
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Huduma za Afya
  • Ardhi na mipango Miji
  • Kujua Kodi ya Ardhi
  • Kalambodc blog
  • TEHAMA
  • Kalmbodc Twitter
  • Kalambodc Facebook
  • Kalmbodc Instagram
  • TAMISEMI

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Wakala wa Manunuzi Serikalini
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
  • Mkoa wa Rukwa
  • Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga
  • Manispaa ya Sumbawanga

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Watu waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Matai, Kalambo, Rukwa

    Anuani ya posta: P.o box 03

    Simu ya Mezani: 025-2955212

    Simu ya mkononi: +255 622 858 482

    Email: ded@kalambodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya tovuti
    • Huduma

Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.