Afisa elimu mkoa wa Rukwa Juma Kaponda amesikitishwa na kitendo cha walimu wa shule ya msingi msishindwe kata ya Mwimbi wilaya ya Kalambo kufundisha kipindi kimoja kwa kipindi cha miezi saba mfululizo na kusababisha wanafunzi 27 kati ya 28 kufeli katika mitihani ya upimaji wa darasa la saba ngazi ya kanda.
Ameyasema hayo wakati wa ziara ya ukaguzi hali ya utendaji kazi ya walimu wa shule za msingi na sekondari wilayani humo na kusema katika ukaguzi huo amebaini walimu wa shule hiyo kutofikia kiwango cha ufundishaji wa vipindi darasani ikiwemo baadhi yao kufundisha vindi 6-10 kwa kipindi cha miezi 7.
Aidha ametumia fursa hiyo kuwataka wenyeviti wa serikali za vijiji na kamati za shule kushirikiana na walimu kwa karibu katika kudhibiti utoro wa wanafunzi shuleni ikiwemo kuwachukulia hatua kali za kisheria wazazi na walezi wanaochangia vitendo vya utoro kwa wanafunzi shuleni.
Baadhi ya walimu wilayani humo ambao licha ya kuipongeza serikali kwa kuanzisha utaratibu wa ukaguzi huo wameomba mfumo huo kuwa endelevu ikiwa ni Pamoja na kudhibiti vitendo vya matumizi ya pombe wakati wa masaa ya kazi dhidi yao.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.