Wizara ya afya nchini Tanzania imethibitisha kuwa watu 84 wapya wameambukizwa virusi vya corona na kufikisha idadi ya wagonjwa wa Covid-19 kufikia 254.
Wagonjwa hao wanatoka katika pande zote mbili za Tanzania, Zanzibar.
Kwa upande wa Bara maambukizi ya virusi hivyo sasa yameripotiwa katika mikoa 17, na wagonjwa wapya waliotangazwa Jumanne na Waziri Ummy mwalimu wanatoka mikoa ya Dar es Salaam(33), Arusha (4),Mbeya(3), Dodoma (3), Kilimanjaro(3), Pwani,(3) Tanga(3), Manyara(2), Tabora(1), Ruvuma(2), Morogoro(2) Rukwa(2), Kagera(1), Mara(1) na Lindi (1).
Habari zaidi zilizotolewa Jumatatu jioni na wizara hiyo zinaarifu kuwa watu watatu wapya wamefariki kutokana na sababu zinazohusiana na maradhi ya Covid-19.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo wagonjwa wote walioripotiwa Tanzania bara wanaendelea kupata nafuu isipokuwa wanne ambao wanahitaji uangalizi maalum.
Kufikia sasa katika eneo la Tanzania bara wagonjwa wameambukizwa kama ifuatavyo kwenye mabano
Wagonjwa 23 kati hao 84 waliothibitishwa ni wale waliotolwa na Wizara ya Afya ya Zanzibar Jumatatu.
Hatuazilizochukuliwa kudhibiti maambukizi ni zipi?
Shule zote na vyuo vya elimu vimefungwa mpaka itakapotangazwa ili kuzuia kuenea kwa maambukizi ya corona nchini humo.
Pamoja na kuzuia mikusanyiko yote ya watu wengi yakiwemo matamasha ya muziki, mikutano ya hadhara mbalimbali ikiwemo ya kisiasa.
Magari ya usafiri wa umma hatayakiwi kujaza abiria, na wote lazima wawe wameketi vitini.
Ndege za abiria zimezuiwa kutua nchini humo.
Kuanzia Jumatatu ya Aprili 20 ni lazima kwa wakaazi wote wa Dar es Salaam kuvaa barakoa wanapokuwa maeneo ya umma.
Biashara zote za chakula jijini Dar es Salaam zinatakiwa kufunga bidhaa zao na kutoruhusu watu kula kwenye migahawa.
Awali Bunge la Tanzania lilithibitisha kwamba mmoja wa wabunge wake ameambukizwa virusi vya corona.
Taarifa hiyo imetolewa na naibu spika wa bunge Tulia Ackson japo hakutaja jina la mbunge huyo.
Aliongeza kuwa mbunge huyo anaendelea vizuri na kuongeza kuwa serikali inamuangalia na kumpatia matibabu stahiki.
Kulingana na maelezo ya mbunge huyo alisafiri na kwenda mjini Dar es Salaam hivi karibuni.
Kwa sasa vikao vya bunge hilo vimeahirishwa ili linyunyuziwe dawa ya kuzuia kusambaa kwa maambukizi ya virusi vya corona.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.