Ikiwa imesalia siku moja kwa wanafunzi wa darasa la saba kuanza kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi hapa nchini,mkuu wa wilaya ya Kalambo Julieth Binyura amesema hatasita kuwachukulia hatua kali za kisheria ikiwemo kuwafikisha mahakamani wasimamizi wa mitihani ambao watakiuka maadili ya kazi yao na kufanya vitendo vya undanganyifu wakati wa uendeshaji wa zoezi hilo.
Akiongea ofisini kwake mkuu wa wilaya hiyo Julieth Binyura kupitia mahojiano maalumu na kituo hiki, amesema Jumla ya wanafunzi 3765 wanategemea kuanza kufanya mtihani wao wa kuhitimu elimu ya msingi kuanzia sptember 11,2019 na huku kati yao hao wavulana ikiwa ni 1854na wasichana 1872.
Aidha amewataka wananchi kuendelea kuwaombea kwa mungu wanafunzi wote ili waweze kufanya vizuri mitihani yao na kufaulu vizuri na hatimaye kujiunga na elimu ya sekondari.
Baadhi ya wanafunzi wilayani humo wamesema wamejiandaa vuziri na wanaimani watafanya vizuri mitihani hiyo.
Mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi inategemewa kuanza sptember 11,2019 na kumalizika sptember 12, 2019 katika shule za msingi 97 za wilaya hiyo.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.