Wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari wilayani Kalambo mkoani Rukwa wametakiwa kuwa sehemu ya kuisaidia serikali katika kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa kutoa taarifa za uwepo wa vitendo hivyo kwenye mamlaka husika ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kufikishwa vyombo vya dola.
Hayo yamebainishwa na afisa ustawi wa jamii katika halmashauri ya wilaya ya Kalambo ndugu Nzumbi Ngusa wakati akitoa elimu ya msaada wa kisheria ya Mama Samia kwa wananchi na wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari katika kata Katete na Sopa na kusisitiza wanafunzi kujenga utamaduni wa kutoa taarifa kwenye mamlaka husika pindi wanapokutana na vitendo viovu.
Kampeni ya msaada wa kisheria kwa wilaya ya Kalambo inafanyika katika vijiji 30 ambapo vijiji 21 hadi sasa vimefikiwa na hudumu hiyo.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.