CHAMA cha Wandishi wa Habari mkoani Rukwa (RKPC) kimepata viongozi wapya watakao kiongoza Chama hicho kwa kipindi cha miaka mitano ijayo. Uchaguzi huo umefanyika Jana kwenye ukumbi wa Manispaa ya Sumbawanga ambapo Waandishi wa Habari walitumia demokrasia yao kupitia uchaguzi ambao uliangaliwa na mjumbe wa bodi UTPC Andrew Kuchonjoma na Mwakilishi wa katibu tawala wa mkoa Emmanuel Kakwezi. Mwenyekiti wa Baraza la uchaguzi Cresensia Daimon alimtangaza Swima Ernest kushinda nafasi ya Mwenyekiti kwa kupata kura 17 za ndiyo huku kura 9 za hapana, Makamo mwenyekiti ni Israel Mwaisaka aliyepata kura 13 ,nafasi ya katibu mkuu ilinyakuliwa na Sammy Kisika aliyepata kura 25 za ndiyo ambapo alipata Kura 1 ya hapana kwa kuwa hakua na mpinzani.
Mwenyekiti huyo wa baraza pia alimtangaza Anna Malisa kuwa mtunza hazina kwa kupata kura 19 dhidi ya mpinzani wake Elizabeth Ntambala aliyepata kura 9.
Kwa upande wa kamati tendaji ya RKPC waliochaguliwa ni Zenat Mohammed, Neema Mtuka na Baraka Lusajo.Aidha alidai kuwa katika uchaguzi huo ulikua na Wapiga kura 27 lakini waliopiga kura walikua 26 kwa maana mmoja hakuweza kupiga kura kwa hiari yake.
Baada ya uchaguzi huo Mwakilishi wa katibu tawala wa mkoa Emmanuel Kakwezi aliwataka wale wote waliochaguliwa katika nafasi mbalimbali waende kufanya kile Wanachama wanakitaka kwa mujibu wa sheria kama walivyoaidi wakati wa kugombea nafasi zao.
Na aliwataka wakawe daraja la mahusiano mema Kati ya Waandishi wa Habari wa mkoa Rukwa na serikali ikiwa ni pamoja na Wadau wengine ili kuweza kuyafikia malengo yao kama Waandishi wa Habari na kuwa serikali ya mkoa ipo tayari kuwapatia ushirikiano wa kutosha.
Andrew Kuchonjoma Mwakilishi wa UTPC alidai kuwa uchaguzi umekwisha Sasa wakajenge umoja miongoni mwao huku akiwataka Waandishi Kuacha kuwa omba omba na badala yake waanzishe miradi itakayowawezesha wao kujitegemea.
Mwisho
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.