Mkuu wa mkoa wa Rukwa mh. Joachim Wangabo amewataka wananchi 638,979 wa vijiji vyote 339, Mitaa 167, Kata 96, Tarafa 16, Halmashauri 4 na Wilaya 3 Mkoani Rukwa walioandikishwa kwaajili ya kupiga kura, kujitokeza katika kupiga kura katika uchaguzi mkuu utaofanyika siku ya Jumatano ya tarehe 28 mwezi Oktoba mwaka huu ili kuwachagua Madiwani, Wabunge Pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aidha, Mh. Wangabo ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha wakulima kuwa katika kipindi hiki cha Kampeni wasisahau kuandaa mashamba yao kwaajili ya msimu wa kilimo wa mwaka 2020/2021 na kusisitiza kuwa wananchi wasiegemee sana siasa wakasahau Maisha ya kawaida ambayo ni kilimo kwa wananchi wengi wa mkoa wa Rukwa.
“Wakati huo huo vyote lazima viende Pamoja na maandalizi ya kilimo, si mvua karibu zinanyesha, ni lazima watu wakaandae mashamba yao, tusiegemee sana siasa tukasahau pia kuna Maisha ya kawaida kwetu sisi ni kilimo, kwahiyo ni lazima tuandae mashamba mapema, uchaguzi unapopita mvua zikinyesha tunakwenda kupanda, mvua za kwanza ni za kupandia, kwahiyo vyote tuvibebe, tumeelewana,” Alisistiza.
Mh. Wangabo ameyasema hayo alipotembelea miradi ya Lipa kulingana na Matokeo (EP4R) na Miradi ya Afya na Usafi wa Mazingira (SWASH) inayotekeleza ujenzi wa madarasa na vyoo vya wananfunzi kwa shule za msingi na Sekondari Wilaya Kalambo, Nkasi na Sumbawanga . ambapo wilaya Hizo zimepokea jumla ya zaidi Shilingi bilioni 2 kwa mwaka huu wa fedha ili kutekeleza miradi hiyo.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.