Wananchi Wilayani Kalambo Mkoani Rukwa wametakiwa kuchukua tahadhari ya magonjwa ya milipuko kwa kufuata kanuni za afya ikiwemo kunawa mikono, kusafisha mazingira sambamba na kutumia maji safi na salama.
Hayo yamebainishwa na Maafisa afya wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika Vijiji vya Mpombwe na Ngorotwa Wilayani humo iliyokuwa na lengo la kutoa elimu ya ujenzi wa vyoo bora.
Kwa upande wake Afisa afya ndugu Adam Rwanda ametumia fursa hiyo kuitaka jamii kujenga utamaduni wa kutumia maji safi na salama kwa kuchemsha pamoja na kujenga vyoo bora ili kujikinga na maradhi yasio kuwa ya lazima.
Mtaalamu wa magonjwa ya milipuko Wilayani humo Dkt. Evelyne Ngori amesema kila Mwananchi ana wajibu wa kuchukua tahadhari dhidi ya magonjwa ya milipuko kwa kufuata kanuni zinazotolewa na Wataalamu wa afya ikiwemo kunawa mikono kwa kutumia sabuni na maji tiririka na kuchana na tabia ya kutumia maji ya mito.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.