• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Kalambo District Council
Kalambo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya sekondari
      • Maji
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo na Ushirika
      • Ufugaji na Uvuvi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Mazingira
      • TEHAMA na Uhusiano
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
      • Kituo Cha Afya Matai
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Upimaji wa Viwanja na Mipango Miji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Uongozi na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Ujenzi Uchumi na mazingira
      • UKIMWI
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Mradi unaoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Bajeti ya Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
  • Salary Slip

Wananchi Katika Kijiji Cha Singiwe Waazimia Kuchukua Hatua Dhidi Ya Wazazi Walioshindwa Kutoa Malezi Kwa Watoto Wao.

Posted on: April 4th, 2022

Wananchi katika Kijiji cha Singiwe kata ya Lyowa wilayani Kalambo mkoani Rukwa wameazimia kuchukua hatua kali dhidi ya wazazi na walezi ambao watabainika kushindwa kudhibiti uzurulaji wa watoto wao nyakati za usiku.

Hatua hiyo inakuja baada ya kujitokeza wimbi la watoto kuanzia miaka 3-8 kukutwa mitaani nyakati za usiku wakizurula na wengine kukutwa kwenye kumbi za kuoneshea video huku wazazi wao wakionekana kutokuwa na habari na familia zao.

 Akiongea kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo,Mwenyekiti wa kijiji cha Singiwe  Donard Songolo , alisema kwa kutambua umuhimu wa ulinzi wa watoto wameanza kuchukua hatua dhidi ya wazazi ambao wamekuwa wakishindwa kuwadhibiti watoto wao nyakati za usiku na kuishia kuangalia video kwenye mabanda umiza huku wengine wakilazimika kulala kwa majirani kutokana na ukosefu wa uangalizi.

‘’tunataka wazazi wawe waangalizi na walinzi wa watoto wao hivyo mzazi au mlezi ambae ataonekana kushindwa kumlea mtoto wake atachukuliwa hatua kali za kisheria kwani tumeshuhudia kila siku watoto  hususani kuanzia miaka 3 wanakuwa kwenye sehemu za kuoneshea video muda ambao walipaswa kuwa nyumbani hali ambayo ni hatari. Alisema chongolo

Diwani wa vitimaalmu katika tarafa ya,Matai wilayani humo  Yuster Kajema , alisema lengo la serikali ni kuhakikisha watoto wote wanalindwa ikiwemo kutambua haki zao za msingi , kupatiwa elimu , malazi na mavazi na kwamba kwa kufanya hivyo ndivyo itaonekana kweli tunawalinda.

‘’lengo la serikali ni kuhahakikisha huduma za malezi jumuishi ya watoto zinawafikia watoto wote wenye umri kuanzia miaka (0-8) pamoja na kuzingatia masuala ya jinsia, watoto walio katika mazingira hatarishi kwa mfano watoto wote wenye VVU, Yatima ,watoto wanao umwa sana pamoja na wenye utapia-mlo ,watoto walipo mahabusu ,kambini na wenye changamoto katika ukuaji  wote kwa umoja wao wanapaswa kulindwa na kupata stahiki muhimu.’’alisema Kajema.

Hata hivyo katika kuhakikisha haki za watoto zinatambulika na kutekelezwa, Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizoridhia na kusaini mkataba wa kimataifa wa haki za mtoto na mapendekezo ya kamati Na. 7 ya mwaka 2005 katika kutekeleza haki za watoto.

Matangazo

  • Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga Kidato cha Kwanza 2021-Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo December 18, 2020
  • Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Kidato cha Kwanza 2021-Tanzania Bara December 18, 2020
  • Tangazo Kwa Wafanyabiashara Wote Wilayani Kalambo Kulipa Vibali Vya Kununua Mazao. July 25, 2019
  • Tangazo La Wadaiwa Sugu Wa Kodi Ya Aridhi Viwanja na Mashamba. October 23, 2019
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • Wananchi Katika Kijiji Cha Singiwe Waazimia Kuchukua Hatua Dhidi Ya Wazazi Walioshindwa Kutoa Malezi Kwa Watoto Wao.

    April 04, 2022
  • Watoto Kuanzia Miaka 0-8 Walindwe Dhidi Ya Vitendo Vya Ukatili. Na Baraka Lusajo – Rukwa.

    March 29, 2022
  • Wilaya ya Kalambo Yazindua Operesheni ya Anwani za Makazi

    March 02, 2022
  • DC kalambo ataka wananchi kuwalinda watoto dhidi ya mafuriko

    February 22, 2022
  • Tazama Zaidi

Video

MHE. RAIS SAMIA S. HASSAN AMUAPISHA MAKAMO WA RAIS MTEULE DKT. PHILIP ISDOR MPANGO IKULU CHAMWINO
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Huduma za Afya
  • Ardhi na mipango Miji
  • Kujua Kodi ya Ardhi
  • TEHAMA

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Wakala wa Manunuzi Serikalini
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
  • Mkoa wa Rukwa
  • Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga
  • Manispaa ya Sumbawanga

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Watu waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Matai, Kalambo, Rukwa

    Anuani ya posta: P.o box 03

    Simu ya Mezani: 025-2955212

    Simu ya mkononi: +255 622 858 482

    Email: ded@kalambodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya tovuti
    • Huduma

Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.