Wananchi mkoani Rukwa wameiomba serikali kuweka utaratibu maalumu ambao utawawezesha kutoa ushahidi mahakamani kwa kujirekodi na kutuma video pamoja na vinasa sauti mahakani badala ya kuapa kwa lengo la kusadia watu kupata haka zao kwa wakati.
Wakiongea wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria yaliyofanyika wilayani Kalambo, walisema serikali haina budi kuziwezesha mahakama kwa kuruhusu watu kutuma video pamoja na vinasa sauti na kutumika kama ushahidi wakati wa uendeshaji kesi mahakamani.
Hakimu wa mahakama ya wilaya ya Kalambo Ramadhani Rugemalira ambae alikuwa mgeni rasm kwenye madhimisho hayo, alisema kwa sasa mashauri yote yatatumwa kwa njia ya simu.
‘’katika kupunguza gharama za mashauri kwa wadau ,mahakama imeanzisha huduma ya mahakama inayotembelea {mobile court }alisema Rugemalila.
Alisema hali kadhalika kwa sasa mahakama inatumia mitambo ya kielektroiniki {viedo conferece facility }kuendesha mashauri mbalimbali kwa baadhi ya maeneo hapa nchini.
Alisema mahakama ya Tanzania katika kuhakikisha mashauri ya biashara na uwekezaji yanaisha kwa haraka ,msisitizo mkubwa umewekwa kwenye utatuzi wa mashauri kwanjia ya usuluhishi {Altenative dispute resolusion }
Alisema kwa upande wa mahakama ya mwanzo mashauri yatatakiwa kumalizika ndani ya miezi sita ,mahakama za hakimu mkazi miezi kumi na mbili kwa mwaka mara moja .
Mkuu wa wilaya ya kalambo Julieth Binyura aliwataka wananchi kujenga mazoea ya kufika mahakamani kutoa ushahidi.
‘’wananchi pia ni wadau muhimu katika kuhakikisha kunakuwepo namazingira wezeshi ya biashara na uwekezaji.kunapokuwa na shauri lolote mahakamani zikiwemo kesi za biashara na uwekezaji ni jukumu la wananchi kufika mahakani kutoa ushahidi ili kesi ziweze kufikia maamuzi sahihi na ya haki kwa wakati.’’Alisema Binyura.
Madhimisho ya sheria hufanyika tarehe 6 ya kila mwaka na kwa mwaka huu yalikuwa na kauli mbiu isemayo‘’Uwekezaji na biashara,Wajibu wa mahakama na wadau kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji’’
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.