• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Kalambo District Council
Kalambo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya sekondari
      • Maji
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo na Ushirika
      • Ufugaji na Uvuvi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Mazingira
      • TEHAMA na Uhusiano
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
      • Kituo Cha Afya Matai
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Upimaji wa Viwanja na Mipango Miji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Uongozi na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Ujenzi Uchumi na mazingira
      • UKIMWI
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Mradi unaoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Bajeti ya Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
  • Salary Slip

Wananchi Wausiwa Kutunza Amani Wakati Wa Uchaguzi Na Sio Kuvunja Udugu.

Posted on: August 21st, 2020


Wananchi Mkoani Rukwa wameusiwa kuendelea kuitunza amani ambayo ndio tunu ya taifa letu la Tanzania hasa wakati huu tunaoukaribia kipindi cha Kampeni kwaajili ya maandalizi ya kuwachagua Madiwani katika ngazi ya Kata, Wabunge katika ngazi ya Majimbo pamoja na Rais wa nchi ya Tanzania katika uchaguzi utakaofanyika siku ya Jumatano tarehe 28.10.2020.

Usia huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo alipotembelea baadhi ya vijiji wilayani Nkasi ili kuhamasisha utulivu na kuwaasa kutovunja udugu kwasababu za kisiasa hali itakayowapelekea kushindwa kushirikiana na kufanya maendeleo katika vijiji vyao hasa baada ya kuisha kwa uchaguzi huo na washindi kupatikana.

Aidha amewataka wanaoshiriki katika kampeni hizo kutotumia lugha za matusi na kutanguliza kuheshimiana bila ya kusahau kuwa kinachowaunganisha ni udugu uliopo baina yao na hivyo kutokubali kuvurugwa na kauli za wanaojinadi na wanaohamasisha vurugu katika kampeni zao.

“Niwaombe ndugu zangu wakati wa kampeni, sisi sote ni ndugu, huyu anaweza akawa yupo CHADEMA, huyu NCCR – Mageuzi, yule wa Chama cha Mapinduzi, lakini sisi sote si ndugu, kwanini mpigane ngumi kwasababu ya uchaguzi, kwanini mtoane ngeu wakati wa uchaguzi, uchaguzi unakwisha, mwezi Novemba raisi anasimikwa pale anaapishwa, ninyi si tutaendelea kuwa ndugu? Sasa kwanini muuane kwasababu hiyo?” Alihoji.

“Watu wakija na kampeni zao wakifanya mbwembwe, wakihamasisha kupigana, mkatae mambo ya fujo kwasababu ninyi mnaishi pamoja ni ndugu, hayo mambo yatapita mpaka tena baada ya miaka mitano, kwahiyo mimi natahadharisha kwamba kipindi cha kampeni, kampeni zifanyike za kistaarabu, lakini watu waheshimiane, kusiwe matusi tukijua kwamba sisi ni ndugu,”Alisema.

Kampeni za Uchaguzi wa Mwaka huu zinatarajiwa kuanza tarehe 26.8.2020 huku wabunge mbalimbali wakiendelea kuchukua fomu za Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutoka kwa wasimamizi wa majimbo katika halmashauri mbalimbali na kuzirudisha halikadhalika wagombea Urais 17 wa vyama 17 nchini wamejitokeza kuwania kiti hicho ambacho Mh.Dkt. John Pombe Magufuli anakiwania kwa muhula wa pili.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI October 03, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI September 10, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2023 July 13, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 01, 2023
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • KAMATI YA USHAURI YA MKOA WA RUKWA YARIDHIA MAPENDEKEZO YA KULIGAWA JIMBO LA KWELA.

    March 15, 2025
  • RC RUKWA AWAONYA VIONGOZI WANAOKWAMISHA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI SAMAZI

    March 14, 2025
  • WANAWAKE KALAMBO WAFANYA UTALI WA NDANI

    March 10, 2025
  • TALGWU YATOA MSAADA WA KIBINADAMU KWA WANAWAKE WANAOJIFUNGUA

    March 10, 2025
  • Tazama Zaidi

Video

MHE. RAIS SAMIA S. HASSAN AMUAPISHA MAKAMO WA RAIS MTEULE DKT. PHILIP ISDOR MPANGO IKULU CHAMWINO
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Huduma za Afya
  • Ardhi na mipango Miji
  • Kujua Kodi ya Ardhi
  • Kalambodc blog
  • TEHAMA
  • Kalmbodc Twitter
  • Kalambodc Facebook
  • Kalmbodc Instagram
  • TAMISEMI

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Wakala wa Manunuzi Serikalini
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
  • Mkoa wa Rukwa
  • Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga
  • Manispaa ya Sumbawanga

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Watu waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Matai, Kalambo, Rukwa

    Anuani ya posta: P.o box 03

    Simu ya Mezani: 025-2955212

    Simu ya mkononi: +255 622 858 482

    Email: ded@kalambodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya tovuti
    • Huduma

Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.