Wananchi kutoka vijiji vya kata ya Mwimbi na Katazi wilayani Kalambo mkoani Rukwa wameadhimisha siku ya afya na lishe ya kijiji kwa kujifunza namna ya kuaanda mashamba ya mboga mboga na matunda pamoja na kundaa vyakula vyenye virutubisho kama sehemu ya kupunguza utapiamlo kwa watoto chini ya miaka 5.
Maadhimisho hayo yamefanyika katika kata za Mwimbi na Katazi na kuongozwa na maafisa watendaji wa kata na watoa huduma za afya ngazi ya jamii na zahanati kwa kuhamaisha jamii nmna ya kuandaa vyakula bora na vyenye virubisho .
Hata hivyo kupitia maadhimisho hayo maafisa watendaji kutoka kwenye kata hizo waliwataka wananchi kujenga mazoea ya kutunza mazingira kwa kupanda miti ya kutosha kuzunguka kaya zao ili kuepuka madhara ya nyumba zao kuezuliwa na upepo.
Licha ya hilo waliwataka wananchi kujenga mazoea ya kundaa vitaro vya mboga mboga pamoja na kuwandalia watoto wao vyakula vyenye virutubish.
Hata hivyo maadhimisho ya afya ya kijiji kwa ngazi ya wilaya hufanyika kwa mwezi wa mwisho kila robo inapoisha kwa kutoa elimu kwa wananchi namna ya kundaa vyakula vyenye virutubisho pamoja na kufanya utambuzi wa watoto wenye utapia mlo ikiwa ni pamoja na kuwapatia rufaa watoto wote wanaobainika kuwa na utapiamlo mkali kwenda kwenda kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.