Kamati ya ulinzi na usalama wilayani kalambo mkoani Rukwa imepiga marufuku wafanyabiashara kuuza saruji kinyume na utaratibu na kuonya wanaouza kwa bei ya juu kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
Hatua hiyo imekuja baada ya kujitokeza malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya wafanyabishara kupandisha bei ya sementi kutoka shilingi elfu kumi na sita (16000/=) hadi kufikia kiasi cha shilingi elfu ishirini na moja (21000/=) kwa mfuko wa kilo 50.
Kutokana na na hali hiyo kamati ya ulinzi na usalama wilayani humo imelazimika kutembelea na kukagua maduka yote yanayohusika na uuzaji wa bidhaa hiyo na kuwataka wafanyabiashara hao kuhakikisha sementi yote inauzwa kwa bei elekezi.
Katibu tawala wilayani humo Frank Sichalwe, amewataka wafanyabiashara kuuza sementi kwa bei elekezi na kusema vyombo vya ulinzi na usalama vitaendelea kukagua ili kuweza kubaini watu wanaouza saruji hiyo kwa bei kubwa.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.