WANAWAKE mkoani Rukwa wameiomba serikali kuweka utaaratibu maalumu ambao utasaidia wao kupata mikopo kwa urahisi zaidi pamoja na kuzisimamia taasisi za kifedha{SACOS}ambazo zimekuwa zikitoa mikopo kwa gharama kubwa na hivyo kupelekea wao kushindwa kujikwamua kiuchumi.
Maadhimisho ya siku ya wanawake hufanyika kila mwaka hapa nchini, ambapo kwa mwaka huu maadhimisho hayo kimkoa yamefanyika katika Kata ya Kisumba wilayani Kalambo mkoani Rukwa na huku mgeni Rasmi akiwa ni mkuu wa mkoa huo Mhe. Joachim Wangabo.
Akisoma taarifa fupi mbele ya mgeni Rasmi, mmoja wa wanawake hao Leonala Jailos, amesema serikali haina budi kuwasidia kwa kutoa mikopo yenye riba nafuu kupitia vikundi na majukwaa yao.
Amesema Halmashauri zimekuwa zikitoa fedha kidogo za mikopo hali ambayo imekuwa ikipelekea baadhi yao kukosa mikopo na kujitokeza malalamiko.
Amesema serikali haina budi kuyawezesha majukwaa ya wanawake yaliyopo katika Halmashauri zote nne za mkoa huo na kusema kwa kufanya hivyo kutaongeza uwajibikaji kwa walengwa na hatimaye kujikwamua kiuchumi.
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mhe. Joachim Wangabo ameziagiza Halmashauri zote za mkoa huo kuhakikisha zinatoa mikopo ya wananawake na vijana na huku akiisifu Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo na Manispaa ya Sumbawanga kwa kutoa mikopo hiyo.
‘’Katika mwaka huu wa fedha 2019/20 katika risala zenu hapa mlionesha wazi kwamba fedha mnazopewa na Halmashauri kuwa hazitoshi na hii nitaiona kwa nini hazitoshi, fedha hizo zinatakiwa zitolewe kama sheria inavyo elekeza lakini Halmashauri zetu zimekuwa hazitoi.’’ alisema Wangabo.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.