Wanawake Wilayani Kalambo mkoani Rukwa wametakiwa kujiimarisha kiuchumi kwa kubuni miradi yenye tija ambayo itawawezesha kukopesheka kwa urahisi kupitia fedha za asilimia kumi zinazotolewa na halmashauri.
Hayo yamebainishwa na mkuu wa wilaya ya Kalambo Dkt Lazaro Komba wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake ambayo kwa ngazi ya wilaya yamefanyika eneo la Mwimbi na kuipongeza halmashauri kwa kufanikiwa kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kutoa mikopo bila riba kiasi cha shilingi 93,2000,00.
Sote ni mashahidi kuwa ipo fursa ya uwezeshaji wanawake kiuchumi kupitia mikopo ya asilimia 10 toka halmashauri ambapo kila robo kuna fedha zimekuwa zikitolewa ili kuwawezesha wanawake kiuchumi, ambapo kwa robo ya kwanza na ya pili kwa mwaka wa fedha 2024/2025 jumla ya shilingi 93,2000,00 zilitolewa kwa vikundi 18 vya wanawake.
Licha ya hilo alisisitiza jamii kutowaacha nyuma wanawake na badala yake wanatakiwa kujiamini na kwamba wao wanaweza kujiletea maendeleo kwa kujishughulisha bila utegemezi.
Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani hufanyika muchi 8 kila mwaka, ambapo kwa mwaka 2025 maadhimisho hayo yamefanyika eneo la Mwimbi kwa ngazi ya wilaya kwa kutoa misaada ya kibinadamu kwa watu wenye uhitaji pamoja na wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.