Ephraim M. Moses alizaliwa mnamo tarehe 18/04/1966 katika kijiji cha Mwakaleli Wilaya ya Rungwe.
Marehemu alimaliza shule ya msingi Kandete mwaka 1982, na kujiunga na mafunzo ya Ualimu ngazi ya Cheti daraja B mwaka 1983 na kuhitimu mwaka 1985. Baada ya hapo Marehemu akajiunga na masomo ya Sekondari kama Mtahiniwa binafsi mwaka 1991 hadi 1992. Mwaka 1992 hadi 1994 Marehemu alijiunga na Mafunzo ya ualimu Daraja la IIIA Chuo cha Ualimu Tukuyu. Mwaka 1995 hadi 1996 marehemu alijiendeleza na masomo ya juu ya sekondari kama mtahiniwa binafsi katika kituo cha Shule ya Sekondari Loleza.
Mwaka 1997 hadi 1999 marehemu alijiunga na Elimu ya Stashahada katika chuo cha Elimu Morogoro. Mwaka 2001 hadi 2007, marehemu alijiunga na Chuo Kikuu Huria cha Dar Es Salaam na kupata Shahada yake ya kwanza ya Sanaa ya Elimu. Mwaka 2011-2013 Marehemu alipata Elimu ya Shahada ya Uzamili katika Sanaa ya Maendeleo ya Chuo Kikuu Dodoma.
AJIRA
Marehemu aliajiriwa mara ya kwanza Mwaka 1986-1989 katika shule ya Msingi Ikomelo Rungwe, kisha akahamia shule ya Msingi Lubala Rungwe na baadae akajiendeleza kielimu na kuhamishwa katika Ofisi mbali mbali za Serikali ikiwemo shule ya Sekondari Mwakaleli, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mbeya na Mwaka 2014 Marehemu Ephraim Moses alihamishiwa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo akafanya kazi ya Afisa Elimu Sekondari Wilaya hadi umauti ulipompata Tarehe 28/05/2020.
MAELEZO YA UGONJWA
Marehemu alianza kujisikia vibaya tarehe 27/5/2020 na hali ilipozidi Marehemu Moses alikimbizwa Hospitali ya Mkoa wa Rukwa tarehe 28/5/2020 hapo ndipo umauti ulipomkuta baada ya kulazwa Hospitalini hapo.
Mnamo tarehe 28/05/2020 Jioni mpendwa wetu aliaga Dunia. Merehemu ameacha Mjane na watoto .
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.