Tume huru ya uchaguzi katika jimbo la Kalambo mkoani Rukwa imehitimisha utoaji mafunzo ya kuwajengea uwezo Makarani waongozaji wapiga kura,wasimamizi wasaidizi wa vituo na wasimamizi wasaidizi wa vituo wapatao 1,703 ambao watasimamia uchaguzi katika vituo 408.
Msimamzi wa uchaguzi jimbo la Kalambo Ndugu Ramadhani Mabula ametumia fursa hiyo kuwataka wasimamizi hao kufahamu kuwa uchaguzi ni mchakato unaojumuisha hatua na taratibu mbalimbali za kikatiba na kisheria ambazo hupaswa kufuatwa na kuzingatiwa hasa katika ngazi za vituo husika.
‘’nachukua fursa hii kuwasaa kuwa, Pamoja na uzoefu ambao baadhi yenu mnao katika uendeshaji wa uchaguzi,msiache kusoma Katiba,sheria, kanuni,taratibu, miongozo na maelekezo yanayotolewa na tume. Alisema Mabula.
Aidha alitumia fursa hiyo kuwataka wasimamizi kuzingatia maadili ikiwemo kuzingatia viapo kwa kutunza siri na kujitoa au kutokuwa wanachama wa vyama vya siasa katika kipindi chote cha uchaguzi.
Kwa upande wake afisa uchaguzi katika Halmshauri hiyo Ndugu Laulent Kapimpiti alitumia fursa hiyo kuwataka wasimamizi hao kuzingatia utekezaji wa majukumu, matakwa na masharti ya sheria ya uchaguzi ili kuepuka kuonekana kuwajibika kwenye mamlaka nyingine tofauti na tume katika kipindi hiki cha uchaguzi.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.