Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mh. Carolius Misungwi amewatahadharisha wazazi Pamoja na Watoto wenye tabia ya kuchezea koki za maji katika vituo vyakuchotea maji vilivyopo kwenye vijiji mbalimbali wilayani humo kuwa watalipishwa faini ya shilingi 50,000 kupitia Jumuiya za Watumiaji maji ngazi ya jamii ili miradi hiyo iweze kuwa endelevu na hatimae kuwanufaisha wananchi kwa muda mrefu.
Mh. Misungwi alisema kuwa kumekuwa na tabia ya Watoto kufungua maji na kuyaacha yakimwagika huku wazazi wakiwaacha Watoto haa bila ya kuguswa na vitendo hivyo na kuwakemea hali inayosababisha koki hizo kuharibika mapema na kushindwa kununua nyingine kutokana na uchangiaji hafifu wa michango kutoka kwa wananchi hao na hivyo miradi kupoteza thamani yake.
Hayo yamesemwa katika uzinduzi wa wiki ya maji Wilayani Kalambo, Mkoani Rukwa ambapo Mgeni rasmi wa tukio hilo Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mh. Carolius Misungwi aliweka jiwe la msingi katika Mradi wa maji wenye thamani ya Shilingi 382,768,375.22 katika Kijiji cha Katete wilayani humo. Mradi uliofadhiliwa kwa fedha za mfuko wa maji wa Taifa na kusimamiwa wakala wa Maji safi na Usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA)
Wakati akisoma risala ya ufunguzi wa wiki ya maji kwa mgeni rasmi, meneja wa RUWASA wilaya ya Kalambo Mhandisi Patrick Ndimbo alisema kuwa miongoni mwa changamoto za miradi hiyo kutoendelea ni Pamoja na wananchi kutochangia huduma ya maji kama sera ya maji yam waka 20002 inavyowataka wananchi wanufaika wa huduma ya maji kuchangia gharama za huduma.
“Mheshimiwa Mgeni Rasmi kutokana na uchangiaji hafifu jumuiya za maji zimekuwa zikishindwakudfanuya matengenezo sehemu zinazoharibika, kurudishia vifaa na vipuli na kushindwa kulipa mishahara ya watumishi wa jumuiya za maji kama fundi na Mhasibu. Hali ya kutolipa huduma ya maji itasababisha miradi ya maji kushindwa kujiendesha na hivyo kufa mapema,” Alisema.
Kwa upande wao wananchi wa Kijiji hicho walitoa shukrani zao kwa Rais Dkt. John Pombe magufuli kwa kuwapatia mradi huo ambao umewakomboa na hivyo kuwapunguzia muda wa kwenda kufuata maji katika maeneo hatarishi.
Miradi inayoendeshwa na RUWASA katika Wilaya ya Kalambo inahudumia wananchi 146,973 kati ya 267,223 sawa na asilimia 55 huku Kauli mbiu ya Wiki ya Maji mwaka huu inasema “Thamani ya Maji kwa Uhai na maendeleo.”
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.