Wavuvi watatu katika kijiji cha kilewani kata ya Kasanga wilayani Kalambo mkoani Rukwa wamekamatwa wakati wakivua samaki kwenye ziwa Tanganyika kinyime na sheria.
Wavuvi hao wamekamatwa kutokana na kukiuka agizo la serikali lililotolewa hivi karibuni juu ya kupumzishwa kwa ziwa na shughuli za uvuvi kwenye ziwa tanaganayika.
Afisa uvuvi wilayani humo Abdul Balozi, amesema wavuvi hao wamekamatwa nyakati za usiku wakati wa doria iliofanywa na kikosi kazi maalmu kinacho shirikisha maafisa uvuvi wa halmashauri na kituo cha doria Kasanga na kwamba watumiwa wamekamatwa wakiwa na nyavu za kololo na kusema zoezi hilo ni endelevu na watu watakao bainika kufanya hivyo watafikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.