Mwenyekiti wa halmashauri ya Kalambo Mkoani Rukwa Daudi Sichone amewataka watendaji wa kata na vijiji wilayani humo kufanya kazi kwa weledi ili kufikia malengo ya serikali katika kuwahudumia wananchi.
Ameyasema hayo kupitia kikao cha baraza la kazi la kujadili taarifa za kata kwa kipindi cha robo ya pili kwa mwaka 2023/2024 kilichofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo februari 15/2024 na kusisitiza watendaji kushirikiana kwa karibu na madiwani katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Awali akiongea kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Sundy wambura ambaye ni afisa maendeleo ya jamii wilayani humo, ametumia fursa hiyo kuwataka watendaji kujikita zaidi katika ukusanyaji wa mapato ya ndani ili kufikia malengo ya serikali katika ukamilishaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.