Watendaji wa serikali za vijiji na kata wilayani Kalambo mkoani Rukwa wamepatiwa mafunzo ya mfumo wa Upimaji na utendaji kazi wa taasisi ya (PIPMIS) na yale ya mfumo wa upimaji wa utendaji kazi kwa watumishi wa umma (PEPMIS).
Mafunzo hayo yameongozwa na maafisa kutoka ofis ya utumishi makao makuu Dodoma na kufanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkurugezi mtendaji ambapo wamesema mafunzo hayo yanalenga kuimalisha uwazi katika utendaji wa shughuli za serikali na kuongeza uwezo wa kiutawala na usimamizi wa rasilimali fedha,upangaji bajeti na usimamizi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo na tathimini ya athari za mipango mbalimbali ya kimaendeleo kwenye taasisi za umma.
Baadhi ya watumishi wa umma wilayani humo wameipongeza serikali kwa kuja na mpango wa utoaji mafunzio hayo na kwamba yatawezesha kuongeza uwajibikaji na kupunguza gharama za usafiri.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.