Uongozi wa Halmashauriya wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa umesema hautasita kuwachukulia hatua kali za kisheria ikiwemo kuwafikisha mahakamani watendaji wote wa vijiji na kata ambao watashindwa kuwasilisha fedha benki za mapato ya ndani na kukaa nazo majumbani kinyume na utaratibu.
Akiongea kupitia mwendelezo wa vikao kazi vilivyofanyika katika tarafa za Ulumi na Mambwenkoswe,Katibu Tawala wilayani humo,Frank Sichalwe, amesema baadhi ya watendaji wamekuwa wakikyuka madili yao ya kazi na kutumia fedha katika matumizi yao binafusi.
‘’acheni mtindo wa kukaa na fedha za makusanyo majumbani mwenu, baada ya uchaguzi tutaanza kukagua mtendaji mmoja baada ya mwingine na atakae bainika atachukuliwa hatua kali za kisheria.alisisitiza sichalwe.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.