Hayo yamebainika kupitia kikao maalumu kilichofanyika katika tarafa ya mwimbi wilayani humo,ambapo wamebainisha kuwa baadhi ya viongozi wa serikali za vijiji wamekuwa wagumu kutoa ushirikiano hususani wakati wa ukusanyaji mapato na hivyo kupelekea mapato kutoroshwa na baadhi ya wafanyashara.
Waendapo serikali ikitoa asilimia hizo ushirikiano baina yao na viongozi wa vijiji utaimalika na vyanzo vyote vya mapato vitathibitiwa .
Mchael Mazila mtendaji wa kata ya ulumi,alisema wenyeviti wa vijiji ndio nguzo kuu katika maeneo yao hivyo endapo kikiwa na ushirikiano wa kutosha mapato ndani ya halmashauri yataongezeka kwa kasi kubwa.
Bahati chapasi mtendaji wa kijiji cha,Mwimbi alisema serikali haina budi kuangalia namana ya kuboresha miundimbinu ikiwemo barabara kwa lengo la kuawezesha wafanyabiashara kupitisha magari yao kwa urahisi zaidi
Mkurugezi mtendaji wilayani humo Msongera Palela amesema halmashauri imejipanga kulipa madeni yote hususani ya asilimia za vijiji na kusema kufikia mwezi wa tisa vijiji vyote vitakuwa vimelipwa.
‘’hapo awali halmashauri ilikuwa na madeni mengi hivyo mzigo ulikuwa mkubwa na kushindwa kulipa asilimia za viijiji kwa wakati lakini tunaimani kufikia mwezi wa tisa vijiji vyote vitakuwa vimelipwa’’alisema msongera.
Afisa tarafa ya Mambwenkoswe Mpapalika mfaume alitumia fulsa hiyo kuwataka wananchi kuendeleaa kuheshimu maamuzi ambayo yamekuwa yakitolewa na mabaraza kutokana kwamba mabaraza yote yapo kisheria.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.