Watia nia 158 wa ubunge na udiwani wilayani Kalambo mkoani Rukwa wamejitokeza kuwania nafasi hizo na watia nia 12 kati hao wamejitokeza kuwania nafasi ya ubunge huku wanachama 110 wakijitokeza kuwania nafasi ya udiwani ngazi ya kata.
Katibu Mwenezi wilayani humo Ndugu Davidi Pondela ,amesema licha ya hilo wanawake 36 wamejitokeza kuwania nafasi ya viti maalumu huku vijana wapatao sita jinsia ya kiume wakijitokeza kuwania nafasi ya ubunge.
Licha ya hilo miongoni mwa wanachama waliojitokeza kuwania nafasi ya ubunge ni pamoja na Davidi Emmanuel Mwanakatwe, Dr Gaspar Peter Mwembezi, Edifonsi Joackim Kanoni, Edson Athanas Makalo,Festus Nichoraus Mitimingi, Florence William Sitima, Fortunatus Elias Mpangamila, Josephat Sinkamba Kandege,Prof. Samwel Victor, Selgius Severine Ntech, Remigius John Kasochela, Timoth Jasson Ngambeki.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.