Mkuu wa wa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa Lazaro Komba amewataka wananchi wilayani humo kuondoa fikra potofu juu ya zoezi la chanjo ya polio ambalo linatarajiwa kuanza kutolewa kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5 wapatao 111524 na kuwataka wataalamu wa afya kuhakikisha wanajikita katika kutoa elimu kwa wananchi ili kuwezesha zoezi hilo kufanikiwa.
Ameyasema hayo kupitia kikao cha afya ya msingi kilichofanyika katika wilayani humo na kuelezea kuwa katika zoezi la chanjo ya awamu ya tatu zoezi hilo lilifanikiwa kwa asilimia mia moja na kwamba watoto wapatao 8486 walipatiwa chanjo ya polio.
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya afya ya msingi wilayani humo wameipongeza serikali kwa kujari afya za watoto wao na kusisitiza watalaamu kujikita katika kutoa elimu maeneo ya mipakani kutokana na maeneo hayo kuwa na mwingiliano mkubwa wa watu.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.