Mkuu wa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa Lazaro Komba amesema watoto 250 wenye umri chini ya miaka 5 wamegundulika kuwa na ugonjwa wa Surua na lubella katika vijiji 10 vya wilaya hiyo ambapo watoto 16 kati yao wametokea katika kijiji cha Msanzi.
Aliyasema hayo wakati uzinduzi wa kampeni ya chanjo ya Surua na Rubella uliofanyika kwa ngazi ya wilaya katika kijiji cha Msanzi wilayani humo na kubainisha kuwa Halmashauri ya Kalambo ilipata mgonjwa wa kwanza wa Surua / Rubella Januari 2023 katika kijiji cha Mlenje kata ya Legezamwendo na baadaye kuenea hadi Septemba 2023 katika maeneo mengine ikiwemo vijiji vya Tunyi, Ilonga,Legezamwendo, Mambwekenya, Limba, Mkowe,Samazi ,Kilewani, Kapele, na Msanzi.
‘’Jumla ya watoto kumi na sita 16 walibainika kuwa na ugonjwa wa surua/Rubella , walipatiwa matibabu mapema na hatimaye kurudi katika hali zao za kawaida za kiafya na hakuna vifo ambavyo vilijitokeza’’ alisema komba
Awali akiongea wakati uzinduzi wa kampeni hiyo mganga mkuu wa Halmashauri hiyo Dkt Emmanuel Mhanda, alisema serikali kupitia wizara ya afya kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo imeandaa kampeni ya kitaifa ya kutoa chanjo ya Surua na Rubella kwa watoto kuanzia miezi 9 hadi 59 ili kuwakinga watoto wote ambao wapo kwenye hatari ya kupata magonjwa hayo ambapo watoto 42,805 wanatarajiwa kufikiwa na kampeni hiyo.
‘’Surua na Rubella ni magonjwa yanayoweza kukingwa kwa chanjo pekee .chanjo hii hutolewa dozi mbili , dozi ya kwanza ni pale mtoto anapofikisha umri wa miezi 9 na dozi ya pili anapewa mtoto anapofikisha miezi 18 katika utaratibu wa kawaida ‘’ alisema Mhanda.
Hata hivyo baadhi ya madaktari wilayani humo akiwemo Abdulkharim Juma, alisema ugonjwa huo unasababishwa na virusi vinavyoenezwa kwa njia ya hewa na kwamba ugonjwa huo unaweza kumpata mtu wa rika lolote na kwamba huathiri zaidi watoto chini ya miaka mitano ambao hawajapata chanjo ya surua /Rubella.
‘’Dalili za ugonjwa wa surua na Rubella ni pamoja na kupata homa ,mafua,kikohozi ,macho kuwa mekundu na kutoa majimaji na vipele vidogo ambavyo huanza kwenye paji la uso , nyuma ya masikio na kusambaa usoni na mwili mzima.
Awali akiongea na wakazi wa kijiji cha Msanzi katibu tawala wilayani humo Servin Ndumbalo , aliwataka wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ili waweze kupata kinga dhidi ya magonjwa yanayoweza kuzuilika kwa chanjo ikiwemo Surua na Rubella.
Baadhi ya wakazi wa wilaya ya Kalambo akiwemo Patrick Sichone wameipongeza serikali kwa kuanzisha kampeni ya chanjo hiyo na kwamba itawawezesha kuondokana ugonjwa huo.
Hata hivyo, timu za utoaji wa chanjo zimeanza kutoa huduma za afya , mashuleni , sokoni , makanisani ,miskitini na kwenye maeneo mengine yenye mikusanyiko huku lengo likiwa ni kufikia watoto 42,805 wenye umri kati ya miezi 9 hadi 59.
Mwisho…..
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.