Mkoa wa Rukwa unakadiriwa kuwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano wapatao 264,068 huku waliosajiliwa na kupata vyeti vya kuzaliwa ni asilimia tano pekee katika mwaka 2021.
Akizungumzia hilo Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joseph Mkirikiti ameeleza kutoridhishwa kwake na takwimu hizi huku akisisitiza kuwa kushindwa kusajili watoto wanaozaliwa katika kaya kunakwamisha upangaji wa mipango ya maendeleo ya mkoa na taifa.
"Hivyo ni matumaini yangu kuwa mpango huu wa usajili wa watoto wa umri chini ya miaka mitano (U5BRI) utawezesha mabadiliko chanya na ni lazima tuhakikishe kila mtoto anayestahili anapata huduma bila usumbufu," alisisitiza.
Mkirikiti alitoa kauli hiyo wakati akifungua semina ya viongozi wa wilaya na mkoa kuhusu Mpango wa Usajili wa Watoto wa umri chini ya miaka mitano (Underfive Birth Registration Initiative-U5BRI) iliyofanyika katika Mji wa Sumbawanga ikiratibiwa na Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA).
Alisisitiza kuwa umuhimu wa cheti cha kuzaliwa ni mkubwa sana kwa wananchi ambao wanavihitaji kama uthibitisho wa umri na taarifa mbalimbali wakati wa kupatiwa huduma kama za elimu, afya na ajira.
"Kumekuwa na tabia ya wananchi kufatilia vyeti mara kinapohitajika hivyo kusababisha mlundikano mkubwa katika Ofisi za RITA wakati wa mazoezi maalumu. Tuwahimize wananchi wote walio na watoto wa umri huu na wana sifa stahiki kutumia fursa hii na wakishavipata wavitunze vizuri mahali salama kwani matumizi yake ni endelevu" alieleza.
Kwa upande wake, Kaimu mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa RITA Emmy Hudson alisema kwa mujibu wa sensa ya watu na Makazi ya mwaka 2012 kwa mkoa wa Rukwa ni asilimia tano (5) tu ndio wamesajiliwa na kuwa na vyeti hivyo kwa zoezi litakaloanza limelenga kuhakikisha watoto wote wasio na vyeti vya kuzaliwa wanasajiliwa.
" Hivyo inawezekana wengine walikuja na watoto wa umri chini ya miaka mitano ambapo kwa mujibu wa Sheria ya Usajili wa Vizazi na Vifo, Sura ya 108 , watoto hao hawastahili kusajiliwa kwani wamezaliwa nje ya mipaka ya Tanzania" alisititiza .
Naye Meneja Utambuzi wa watu na Usajili toka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Julien Mafuru alisema watahakikisha watoto wanaosajiliwa ni wale tu wenye sifa za uraia na kuwa tahadhali zote zimechukuliwa kwa halmashauri za mkoa wa Rukwa.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.