Wadau wa kupinga na kukemea matukio ya ukatili wa kijinsia mkoani Rukwa wameitaka jamii kuendelea kukemea vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto wenye umri chini ya miaka 8 kwa kutoa taarifa kwenye vyombo husika ili kuchukuliwa hatua za kisheria
Wakiongea katika nyakati tofauti,wamesema matukio ya ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto yamepungua kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na awali ambapo watoto walikuwa wakiteswa na kunyimwa haki zao zamsingi ikiwemo elimu.
Wamesema licha ya kuwepo kwa mafanikio hayo lakini bado mashirika yana nafasi ya kuendelea kupinga na kukemea matukio hayo kwa kutoa elimu katika jamii ili kuweza kutokomeza kabisa.
Mkuu wa polis wilayani Nkasi David Mpasya, amesema changamoto kubwa imekuwa kwa wazazi kuto toa ushirikino wakati wa uendeshaji kesi mahakamani na kusema ni vyema mashirika yakaendelea kutoa elimu kwa wazazi juu ya umuhimu wa elimu.
Mratibu wa kupinga mimba za utotoni kupitia shirika lisilo la kiserikali la GCDE bwana Antoni Komba, amesema matukio ya ukatili wa kijinsia yamepungua kwa kiwango cha juu kwani hata vipigo kwa wanafunzi mashuleni vimepungua na kusema swala hili limefanikiwa kwa kiwango cha juu kutokana na elimu iliyotolewa kwa wananchi na mashirika husika.
Hata hivyo mashirika ya ECD yamekuwa miongoni mwa mashirika yaliyosadia kupunguza matukio ya kijinsia kwa kutoa elimu kwa wananchi kupitia vyombo vya habari na midaharo.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.