• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Kalambo District Council
Kalambo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya sekondari
      • Maji
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo na Ushirika
      • Ufugaji na Uvuvi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Mazingira
      • TEHAMA na Uhusiano
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
      • Kituo Cha Afya Matai
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Upimaji wa Viwanja na Mipango Miji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Uongozi na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Ujenzi Uchumi na mazingira
      • UKIMWI
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Mradi unaoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Bajeti ya Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
  • Salary Slip

Watoto Wa Kike Waomba Mabweni Mashuleni kujengwa

Posted on: October 12th, 2020


WATOTO wameomba kuwepo na Mabweni katika shule za Sekondari ili kuondoa uwezekano wa Watoto hao kwenda kupanga vyumba mjini wawapo shuleni ili kuweza kuondokana na mimba za utotoni.

Ombi hilo limetolewa jana na Wanafunzi wa shule za Sekondari za Mashete,Mtenga,Milundikwa,Mkwamba,Isale,Mkangale,Nkomolo na NkaSI sekondari kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike ambapo wamedai kuwa kitendo cha wao kupanga vyumba mjini ni kichocheo kikubwa cha wao kupata vishawishi vinavyopelekea kupata mimba na kukatishwa masomo yao.

Wakizungumza kwenye mdahalo Maalumu ulioandaliwa na shirika lisilokuwa la kiserikali la Plan International juu ya Matumizi ya mitandao ya kijamii kama ikitumika vibaya inaweza kuwapa madhara ya kupata mimba na ndoa za utotoni bila yao kutegemea walidai kuwa ni kweli lakini kubwa linalowasumbua wao kama Watoto wa kike ni kukaa mitaani badala bwenini ambako kuna uangalizi mkubwa.

Akizungumza kwenye mdahalo huo Adolphina Kapembwa Mwanafunzi wa shule ya sekondari Mkangale alidai kuwa licha ya mitandao ya kijamii kuwa na changamoto kwao,lakini kubwa ni la kukosekana kwa Mabweni ya kutosha mashuleni inayopelekea wengi wao kwenda kupannga vyumba mitaani ambako ukutana na vishawishi vingi ambavyo ukwamisha ndoto zao walizojiwekea katika maisha yao.

Hivyo aliwaomba Wazazi wao,serikali na Wadau wengine kuliona jambo hilo kuwa ni la msingi kwa kuhakikisha kuwa katika shule zote za Sekondari yanajengwa Mabweni ya kutosha kuwawezesha Watoto wote hasa wa kike wanaishi kwenye Mabweni kuliko na uangalizi mkubwa ukilinganisha na mitaani kwenye vishawishi vingi.

Benezeth Mtuka kwa upande wake alisema kuwa Mitandao ya kijamii ni muhimu kwa maendeleo lakini pale inapotumika vibaya ina madhara makubwa hasa kwa Watoto wa kike bali kinachotakiwa ni Wao wenyewe Watoto kujitambua kuwa wao ni nani? Na lengo lao nini wawapo shule na kuwa hilo likiwezekana mimba na ndoa za utotoni zitatoweka kabisa kwa Watoto walio mashuleni.

Mwakilishi wa dawati la jinsia na Watoto Atupele Hance alisema kuwa changamoto kubwa wanayoipata jeshi la Polisi ni kupata ushahidi dhidi ya vitendo hivyo na kuwa kama Watoto wenyewe wangekua Wawazi vitendo hivyo vya mimba za Utotoni ingekua ni ndoto.

Alisema kuwa kama Wasichana wangekua wanatoa taarifa pale wanapotongozwa ingeasaidia sana kuwawekea ulinzi lakini kitendo cha kukaa kimya kinawapa nguvu Wanaume cha kuendelea kuwarubuni na mwisho wa siku wanaingia mitegoni.

Meneja miradi wa Plan International Williamu Mtukananje alisema kuwa shirika lake kwa kushirikiana na serikali wamekua katika vita hiyo kubwa ya kukabiliana na mimba za Utotoni na kuwa hivi sasa vita hiyo imeeleweka kwa jamii bali kinachotakiwa sasa ni ushirikiano toka kwa wazazi kwa maana ndiyo wamekua wakiharibu kesi hizo pindi ziendapo mahakamani

mwisho

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI October 03, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI September 10, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2023 July 13, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 01, 2023
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • KAMATI YA USHAURI YA MKOA WA RUKWA YARIDHIA MAPENDEKEZO YA KULIGAWA JIMBO LA KWELA.

    March 15, 2025
  • RC RUKWA AWAONYA VIONGOZI WANAOKWAMISHA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI SAMAZI

    March 14, 2025
  • WANAWAKE KALAMBO WAFANYA UTALI WA NDANI

    March 10, 2025
  • TALGWU YATOA MSAADA WA KIBINADAMU KWA WANAWAKE WANAOJIFUNGUA

    March 10, 2025
  • Tazama Zaidi

Video

MHE. RAIS SAMIA S. HASSAN AMUAPISHA MAKAMO WA RAIS MTEULE DKT. PHILIP ISDOR MPANGO IKULU CHAMWINO
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Huduma za Afya
  • Ardhi na mipango Miji
  • Kujua Kodi ya Ardhi
  • Kalambodc blog
  • TEHAMA
  • Kalmbodc Twitter
  • Kalambodc Facebook
  • Kalmbodc Instagram
  • TAMISEMI

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Wakala wa Manunuzi Serikalini
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
  • Mkoa wa Rukwa
  • Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga
  • Manispaa ya Sumbawanga

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Watu waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Matai, Kalambo, Rukwa

    Anuani ya posta: P.o box 03

    Simu ya Mezani: 025-2955212

    Simu ya mkononi: +255 622 858 482

    Email: ded@kalambodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya tovuti
    • Huduma

Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.