Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Kalambo mkoani Rukwa Ndugu Ramadhan Mabula, amesema watu 157,253 ambao walijitokeza kujiandikisha katika Daftari la kudumu la wapiga kura,wanatarajia kupiga kura Oktoba 29 /2025 katika vituo 408 ili kumchagua Rais, Wabunge na Madiwani.
Amesema uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani utafanyika siku ya Jumatano tarehe 29. Oktoba 2025 na kwamba vituo vitafunguliwa kuanzia saa moja kamili (1;00) Asubuhi na kufungwa saa kumi kamili (10;00) jioni.
Aidha ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi wote kupitia taarifa hizo ili kutambua mapema vituo vitakavyo tumika kupiga kura ikiwemo kuona mifano ya karatasi za kupigia kura.
‘’kwa mpiga kura aliyepoteza kadi yake ambaye alijiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura , ataruhusiwa kupiga kura endapo atafika katika kituo alichopangiwa akiwa na leseni ya udereva au pas ya kusafiria au kitambulisho cha taifa (NIDA) majina ya kitambulisho mbadala atakacho wasilisha yawe yanafanana na yaliyomo kwenye Daftari la kudumu la wapiga kura .’’alisema Mabula.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.