Watu 18 raia wa nchi jirani ya Zambia wanashikiliwa na idara ya uhamiji mkoani Rukwa kwa tuhuma za kuingia nchini kupitia mpaka wa Kasesha wilayani Kalambo bila vibali na huku wananchi wakiitaka idara hiyo kuwachukulia hatua kali za kisheria ikiwemo kuwafikisha mahakamani watazania waliohusika kuwasafarisha na kuwahifadhi watu hao.
Hatua hiyo imekuja kufuatia idara ya uhamiaji kufanya msako mkali katika mpaka wa Kasesha wilayani Kalambo na kuwakamata watanzania kumi ambao walikamatwa kwa kosa la kuwahifadhi watu ambao ni raia wa nchi jirani ya Zambia kinyume na utaratibu.
Kamishina msaidizi wa uhamiji mkoani Rukwa Elizeus Mshongi, alisema‘’watu kumi na moja ambao ni raia wa nchi jirani ya Zambia wamerejeshwa katika nchi yao kutokana na wengine kuwa wazee na wengine kuwa wagonjwa, na watu wengine saba ambao ni raia wa nchi hiyo walifikishwa katika mahakama ya wilaya ya Kalambo na kuhukumiwa kutumikia kufungo cha miezi sita au kulipa faini ya shilingi laki tano kwa kila mmoja na msako bado unaendelea.alisema Mshongi.
Alisema licha ya hilo watu 6 raia wa nchini Ethiopia wanashikiliwa na idara ya uhamiaji kwa kosa la kuingia nchi bila vibali na kusema watu hao walikamatwa wakiwa na pasipoti za Kenya na huku vitambulisho vyao vikiwa ni vya Ethiopia .
‘’Baada ya kuwapekuwa Zaidi walikutwa na pasipoti zinazoonyesha kuwa walipitia katika kituo cha uhamiaji cha Namanga kilichopo mkoani Arusha lakini baada ya kujiridhisha Zaidi kupitia maafisa uhamiaji waliopo kwenye eneo hilo waligundua walikataa kuwapokea wahamiaji hao na kugundua kuwa pasipoti zao zilikuwa feki’’.alisema Mshongi.
Aidha aliwataka wananchi kuacha kuwahifadhi wahamijia hao nakuahidi kuchukua hatua kali za kisheria kwa watanzania ambao watabainika kuwahifadhi watu kutoka nchini zingine kinyume na utaratibu.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.