KAYA 47 zimebaki bila makazi baada ya nyumba 13 kubomoka kutokana na mvua kubwa iliyonyesha juzi katika kijiji cha kasitu kata ya sopa wilayani kalambo mkoani Rukwa.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baada ya tukio hilo kutokea ,wakazi wa kijiji hicho walisema kuwa mvua hiyo ilikuwa kubwa na imeambatana na upepo mkali ilianza kunyesha majira ya saa nane na dakika arobaini na tano mchana na kusababisha kubomoka nyumba hizo.
Anold Yolam,mkazi wa kijiji hicho alisema kuwa baadhi ya watu ambao nyumba zao zimebomoka wamepewa hifadhi kwa mwenyekiti wa serikali ya kijiji na wengine wamepewa hifadhi kwa majirani na kuiomba serikali iwasaidie.
Naye Jeriko Malema alisema kuwa mvua hiyo ilinyesha kwa muda mfupi lakini iliambatana na upepo mkali na hali itasababisha kubomoka kwa nyumba hizo.
Kwaupande wake ofisa mtendaji wa kijiji hicho Gasper Kateka alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa nyumba 13 zimeanguka na kuwaacha watu 47 bila makazi.
Alisema kuwa baadhi ya wananchi ambao nyumba zao zimebomoka wamepewa hifadhi kwa mwenyekiti wa kijiji na wengine kwa majirani wakati wakisubiri msaada zaidi.
Mwenyekiti wa kijiji hicho John Sizo alisema kuwa wananchi wengine ambao hawakupatwa na janga hilo wanawajibu wa kuwasaidia watu waliopatwa na maafa hayo.
Mkuu wa wilaya ya Kalambo Just Binyura alisema kuwa kutokea tukio hilo limetokana na wananchi kutojenga nyumba imara na zenye ubora kwani ndizo zitakazo saidia kuondokana na adha hiyo.
Alisema nyumba nyingi zilizo athirika hazikuwa zimejengwa kwa kufuata taratibu za ujenzi bora hivyo wananchi wanapaswa kuwashirikisha wataamu wa halmashauri pindi wanapo jenga nyumba zao ili wawape ushauri wa namna ya kujenga nyumba bora.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.