• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Kalambo District Council
Kalambo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya sekondari
      • Maji
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo na Ushirika
      • Ufugaji na Uvuvi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Mazingira
      • TEHAMA na Uhusiano
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
      • Kituo Cha Afya Matai
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Upimaji wa Viwanja na Mipango Miji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Uongozi na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Ujenzi Uchumi na mazingira
      • UKIMWI
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Mradi unaoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Bajeti ya Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
  • Salary Slip

Watu 49 Wawekwa Karantini Mkoani Rukwa Huku Kati Yao Watanzania Wakiwa Ni 36 Na Wageni 13.

Posted on: April 10th, 2020


Watu 49 wamewekwa karantini mkoani Rukwa kati yao watanzania wakiwa ni 36 na wageni 13 baada ya kupita katika bandari na mipaka rasim ya mkoa huo huku mkuu wa mkoa huo Joachim wangabo akipiga malfuku bandari bubu zilizopo  kwenye mwambao wa  ziwa Tanganyika kutumika.

Mh Wangabo alisema hadi sasa mkoa wa Rukwa umewaweka Karantini watu 49 ambapo kati ya hao watanzania 36 na wageni 13 ambao walipita katika bandari na mipaka rasmi ya mkoa huo na kusisitiza kuwa katika utekelezaji wa kuwaweka watu Karantini hauangalii uraia wa mtu wala hadhi yake, na kuongeza kuwa inachokijali serikali ni usalama wa wananchi wake dhidi ya ugonjwa hatari wa Corona.

Hivyo amewataka viongozi wa serikali za vijiji na kata mkoani hapa  kuwaelimisha wananchi kuwakataa wageni wasiotumia mipaka na bandari rasmi kuingia katika nchi kwani kutofanya hivyo kutailetea nchi maafa makubwa na hivyo na hivyo kuwataka viongozi na wananchi kuacha matumizi ya bandari bubu zilizopo katika vijiji vya mwambao wa ziwa Tanganyika.

“Waende wakapite katika maeneo ambayo ni rasmi, waje hapa kwenye bandari ya Kabwe, wapite hapo na taratibu nyingine za kiafya zitafanyika, lakini sio kwenye bandari bubu huku, bandari bubu ni marufuku kutumika, ndani ya wilaya hii ya Nkasi kuna bandari bubu 46, Nkasi peke yake na katika kata zenu mbili hizi, ya Korongwe na Kabwe kuna bandari bubu 13, ndio maana nikasema viongozi ninyi wa kata mbili hizi mje hapa, ili muone umuhimu wa kuzuia watu kiholela holeal kuja kwenye bandari hizi bubu,” Alisisitiza.

Mh. Wangabo ameyasema hayo wakati wa kikao na wenyeviti wa vitongoji na vijiji vyenye bandari bubu pamoja na watendaji wa kata Kabwe na Korongwe zinazobeba vijiji hivyo katika kikao kilicholenga kutoa elimu ya ugonjwa wa Corona kwa viongozi hao pamoja na kutoa maelekezo ya serikali dhidi ya mapambano ya ugonjwa huo.

Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Uhamiaji Mkoa wa Rukwa Kamishna Msaidizi Elizeus Mushongi alitahadharisha matumizi mabaya ya madaraka ya viongozi hao ambao huwapokea wageni hao na kuwaruhusu kuingia katika nchi bila ya kufuata utaratibu wa serikali na kuongeza kuwa matumizi ya bandari bubu ni haram una hivyo atakayekamatwa anahalalisha matumizi ya bandari hizo hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

“Wageni kutoka nje ya nchi, iwe Kongo, iwe Burundi, iwe Zambia, mnawapokea kule na nyinyi ndio mnakuwa maafisa uhamiaji, mnakuwa maafisa forodha, kila kitu mnamaliza wenyewe kule, sasa kama mtampokea mtu anaumwa ule ugonjwa, ninyi ndio mtakaoanza kuupokea ule ugonjwa kabla ya wote na bila ya kujua mtaenda kuambukiza familia na familia kama dokta alivyosema, niwaombe sana msipokee watu kutoka nje ya nchi kama hawajapita katika vituo vilivyoainishwa kisheria,” Alisema.

Aidha wakati akitoa salamu zake kwa mkuu wa mkoa, Diwani wa Viti Maalum Mh. Christina Simbakavu alisema kuwa kuna baadhi ya watu wenye ndugu zao nchi ya jirani ya Kongo huwa na kawaida ya kuingia katika vijiji hivyo nyakati za usiku na ndugu zao huwapokea katika utaratibu ambao unaweza kuhatarisha maisha yao.

“Kuna boti zinazoingia usiku kama alivyotamka mjumbe wa Kijiji cha Kalila, zile boti zinaingia lakini wenyeji wenye ndugu zao kutoka nchi jirani ya kongo wanawapokea katika mazingira ambayo sio Rafiki sana na hawatoi taarifa, na hili nalo linafukuta lakini hatujapata uhakika uliowazi, tunajaribu kuongea na wananchi kuwa tusipokee wageni wa aina yoyote na nawaomba viongozi wangu tuhamasishe utumiaji wa maji na sabuni kunawa na katika nyumba zetu tuweke vifaa hivyo,” alisema.

Naye Diwani wa Kata ya Korongwe Mh. Venus Bamilitwaye wakati akitoa neno la shukurani ka mkuu wa mkoa wa rukwa aliwasisitiza viongozi wa kata hizo kuhakikisha wanashirikiana na wananchi katika kulinda bandari bubu pamoja na kuzuia uingiaji wa kiholela wa wageni jambo ambalo ni hatari kwa afya ya wananchi wa mkoa wa Rukwa na Tanzania.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI October 03, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI September 10, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2023 July 13, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 01, 2023
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA KALAMBO YAFIKIA ASILIMIA 120 UKUSANYAJI WA MAPATO.

    June 27, 2025
  • HALMASHAURI YA KALAMBO YAFIKIA ASILIMIA 120 UKUSANYAJI WA MAPATO.

    June 27, 2025
  • KAMATI YA USHAURI YA MKOA WA RUKWA YARIDHIA MAPENDEKEZO YA KULIGAWA JIMBO LA KWELA.

    March 15, 2025
  • RC RUKWA AWAONYA VIONGOZI WANAOKWAMISHA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI SAMAZI

    March 14, 2025
  • Tazama Zaidi

Video

MHE. RAIS SAMIA S. HASSAN AMUAPISHA MAKAMO WA RAIS MTEULE DKT. PHILIP ISDOR MPANGO IKULU CHAMWINO
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Huduma za Afya
  • Ardhi na mipango Miji
  • Kujua Kodi ya Ardhi
  • Kalambodc blog
  • TEHAMA
  • Kalmbodc Twitter
  • Kalambodc Facebook
  • Kalmbodc Instagram
  • TAMISEMI

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Wakala wa Manunuzi Serikalini
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
  • Mkoa wa Rukwa
  • Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga
  • Manispaa ya Sumbawanga

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Watu waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Matai, Kalambo, Rukwa

    Anuani ya posta: P.o box 03

    Simu ya Mezani: 025-2955212

    Simu ya mkononi: +255 622 858 482

    Email: ded@kalambodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya tovuti
    • Huduma

Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.