Wananchi wa kijiji cha Mbuluma wilayani Kalambo mkoani Rukwa wamemuua kwa kumchoma moto Amosi Kapufi miaka 22 mkazi wa kijiji cha Myunga baada ya kumchoma kisu mtoto wa dada yake aliefahamika kwa jina la Catherin Kakusu na kufariki dunia papo hapo kutokana na wivu wa kimapenzi.
Imedaiwa kuwa marehemu kabla ya kifo chake alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na binti huyo ambae alikuwa akiishi katika kata jirani na maeneo anayoishi wilayani humo.
Kwa mujibu wa mzazi wa kijana huyo, Bosko Kapufi, amebainisha kuwa kabla ya kifo chake, marehemu alikuwa ameelekea kwenye kata ya Mbuluma kwa lengo la kuwaona ndugu zake, ambapo baada ya kukutana na binti huyo alianzisha vurugu na kumchoma kisu binti huyo katika sehemu za tumbo na shingoni na kufariki dunia.
Amesema kufuatia tukio hilo wananchi kutoka sehemu mbalimbali walikusanyika kisha kumpiga kijana huyo .
“Kifo cha kijana wangu kimenisikitisha sana kwani kijana huyu alikuwa mwaka wa kwanza katika chuo kikuu cha Sauti hivyo sote tumepata hasara kubwa sisi kama wazazi lakini pia serikali”. Alisema Kapufi
Mkuu wa wilaya ya Kalambo Julieth Binyura , alikiri wazi kutokea tukio hilo na kusema tukio hilo lilitokea baada ya watu hao kutofautiana na kuwasihi wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi .
“Tukio hili limetusikitisha sana wananchi wa Kalambo kwani kitendo cha kufanya mauaji ni kosa, hivyo niwatake wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi na badala yake kunapotokea tatizo waende kwenye uongozi husika”. Alisisitiza Binyura.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.