Watumishi wa Umma wilayani Kalambo mkoani Rukwa wameungana na watu wengine katika kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya mashujaa kwa kufanya usafi kwenye majengo ya hospitali ya wilaya ili kuendeleza kampeni ya usafi wilayani humo.
Zoezi hilo liliongozwa Mkuu wa wilaya hiyo Lazaro Komba ambae alisisitiza kuwa zoezi hilo ni endelevu kwa kila siku ya mwisho wa mwezi ili kukabiliana na magonjwa ya milipuko ikiwemo kipindupindu na magonjwa kuhara.
Komba alisisitiza wananchi kujenga mazoea kufanya usafi wa mazingira kuzunguka maeneo yao husika kwa lengo la kuifanya wilaya kuwa safi muda na wakati wote.
‘’Kimsingi leo tumekutana kufanya usafi hapa kwenye majengo ya Hospitali ya wilaya Kalambo kama sehemu ya kuadhimisha kumbukizi ya siku ya mashujaa na maadhimisho haya kwa ngazi ya kitaifa yanafainyika mkoani Dodoma’’ alisema komba.
Mapema akiongea na Watumishi wa umma wakati wa shughuli za usafi kwenye maeneo hayo ,Mkurugezni mtendaji wa Halmshauri hiyo Shafi Mpenda alisema Halmashauri imeanzisha sheria ndogo ili kudhibiti uchafuzi wa mazingira ikiwemo kuhakikisha kila mwananchi anakuwa na choo bora.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.