Watumishi wa umma wilayani Kalambo mkoani Rukwa wameungana na watu wengine duniani katika kuadhimisha siku ya usafi kwa kufanya usafi kwenye ofisi za taasisi za umma ikiwemo hospitali ya wilaya.
Afisa mazingira wilayani humo Jofrey Mwasomola kupitia shughuli za usafi,amesema wanatarajia kulifanya zoazi hilo kuwa endelevu kwa kuhimiza jamii kufanya usafi kila siku ya jumamosi ya mwisho wa mwezi na kwamba watakaoshindwa kufanya usafi kwenye maeneo yao watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kupigwa faini ya shilingi elfu hamsini (50000/=).
Afisa afya wa Halmashauri hiyo Queen Nyahenga ameitaka jamii kuweka utaratibu wa kujenga vyoo bora ili kujiepusha na magonjwa ya milipuko ikiwemo kipindupindu na maambukizi ya virusi vya polio.
Maadhimisho ya siku ya usafi duniani hufanyika kila ifikapo septemba 16 ya kila mwaka ambapo Halmashauri ya Kalambo imeadhimisha siku ya usafi kwa kufanya usafi kuzunguka maeneo ya taasisi za umma.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.