Uongozi wa Halmashauri ya Kalambo kwa kushirikana na taasisi mbalimbali za serikali na binafsi ikiwemo jeshi la polisi,mahakama na Ruwasa zimeungana na watumishi wote wilayani humo katika kufanya mazoezi ya viungo vya mwili kwa kupanda ngazi za Maporomoko ya Kalambo Falls zenye urefu wa mita1600 kwa lengo la kuimarisha afya ikiwa ni pamoja na kujiepusha na magonjwa yasio ya kuambukiza.
Mazoezi hayo yamehusisha taasisi zote za serikali na binafsi wilayani humo pamoja na watumishi wa umma kwa kupanda ngazi za maporomko ya Kalambo Falls ambayo ni ya pili barani afrika kwa urefu kwa mita 235.
Mkurugenzi mtendaji Halmashauri hiyo Msongela Palela, amesema kila mtu anawajibu wa kuwekeza katika mazoezi ikiwa ni pamoja na kutembelea maporomko ya kalambo falls ili kufanya utalii wa ndani.
‘’ kila wiki ya mwisho wa mwezi huwa tunafanya mazoezi ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mh. Makam wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassani, na leo tumefanya mazoezi katika uwanja wa kateka na baadae tukaelekea katika eneo la maporomko ikiwa ni sehemu ya kufanya mazoezi lakini pia kufanya utalii wa ndani ‘’.alisema Msongela.
Katibu tawala wilayani humo Frank Sichalwe, amempongeza mkurugenzi mtendaji kwa kuhamasisha watumishi kufanya mazoezi na kusema hiyo ni hatua nzuri hususani katika ulinzi na uimara wa afya ya kila mmoja.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.