Wakati tukielekea kufanya uchuguzi wa mkuu wa serikali za mitaa hapa nchini, watumishi wa uma mkoani Rukwa wameshauliwa kuendelea kufanyakazi kwa uadilifu na kuzingatia kanuni na miongozo iliowekwa kwa kutekeleza majukumu yao bila kusukumwa na mtu.
Kumekwepo na changamoto ya baadhi ya watumishi kutozingatia kanuni na miongozo ya utumishi wa uma hususani wakati wa utekelezaji wa majukumu yao kwenye maeoneo yao husika na kupelekea baadhi ya kazi kutofanyika kwa ufasaha.
Awali akiongea kupitia madhimisho ya wiki ya utumishi wa uma wilayani kalambo katibu tawala msaidizi mkoani Rukwa Winnie Kijazi alisema kila mtumishi anawajibu wa kufanya kazi kwa bidii kwa lengo la kufikia malengo yaliokusudiwa na serikali.
‘’tunaelekea katika uchaguzi mkuu wa serikali za mitaa hivyo ningependa kila mtumishi awajibike kwa nafasi yake kwa kufanya kazi kwa bidii na kwa kufuata miongozo sahihi iliwekwa na serikali ya jamhuri ya mungano wa Tanzania’’Alisema kijazi.
Dolice Mzigilwa katoka idara ya utawa ofisi ya mkuu wa mkoa ,alisema kila mtumishi anawajibu wa kuheshimu sheria zilizowekwa na jamhuri ya mungano wa Tanzania.
‘’kila mtumishi anawajibu wa kufanyakazi bila kumuonea mtu na kwa kuzingatia maadili ya kazi yake bila kuangalia sura ya mtu au watu’’alisemaMzingilwa.
Dues kaetamu mwangazi ofis ya mkuu wa mkoa alisema kila mtumishi anawajibu wa kujenga mazoea ya kusoma katiba ya jamhuri ya mungano waTanzania ili kuelewa kile kilicho andikwa na kukitendea kazi.
Kaimu mkurugezi mtendaji halmashauri ya wilaya ya kalambo Nikoraus Mlango amewataka watumishi wote kujenga mazoea ya kujaza fomu za opras ambazo zitawasaidia kupanda madaraja kwa wakati.
‘’niwakumbushe tu watumishi wangu kuwa ni muhimu kujaza fomu za opras kutokana na kuwa na manufaa mengi ikiwemo kupima uwezo wa kazi pamoja na kuwasaidia kupanda madaraja kwa wakati’’alisema mlango.
Hata hivyo halmashauri ya wilaya ya kalambo imefanikiwa kubalisha muundo watumishi 52 na huku watumishi 661 barua zao zikiwa zimetumwa kwenye mfumo wa malipo na huku kauli mbiu ya katika madhimisho ya wiki ya utumishi wa uma ikiwa ni uhusiano kati ya uwezeshwaji wa vijana na usimamizi wa masuala ya uhamiaji ,kujenga utamaduni wa utawala bora,matumizi yaTehama na ubunifu katika utoaji wa huduma jumuishi.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.