Afisa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kutoka ofis ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa (TAMISEMI) Damas Makweba amewataka watumishi wa umma mkoani Rukwa kutumia mfumo wa ununuzi wa elekroniki (NeST) kwa udailifu ,uwazi na uwajibikaji ili kufikia malengo ya serikali.
Ameyasema hayo kupitia kikao kazi kilicho jumuisha watumishi wa umma wilayani Kalambo mkoani Rukwa na kusema mfumo huo umelenga kurahisisha upatikanaji wa thamani ya fedha katika ununuzi na ugavi pamoja na ufuatiliaji wa sheria za ununuzi kwenye tasisi za umma.
Aidha Makweba amefafanua nguzo za ununuzi wa umma ambazo zinaweza kutumika kujenga na kuimarisha mfumo wa ununuzi wa kielektroniki ikiwemo usawa na uadilifu kwa wanunuzi na kusema suala la ununuzi linahitaji uadilifu ili kuepusha migongano baina ya mnunuzi na serikali,uwazi na uwajibikaji, thamani inayolingana na ubora pamoja na zabuni za uwazi na ushindani.
‘’wateja wanaweza kufanya manunuzi popote walipo na wakati wowote bila kuhitaji kwenda dukani. Mbali na urahisi, NeST pia hutoa usalama wa malipo. Mifumo ya malipo kwenye NeST ni salama na inalinda taarifa za kibenki za wateja, hivyo kufanya manunuzi kuwa salama zaidi’’alisema makwemba
Aidha amesema katika muktadha wa biashara, matumizi ya NeST yamekuwa na mafanikio makubwa kwani Kampuni nyingi zimekuwa zikitumia mfumo huo kwa kufanya biashara zao kwa ufanisi zaidi na kuvutia wateja wengi Zaidi.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.