HALMASHAURI ya wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa imeanzisha utaratibu wa kuwatambua watumishi wanaofanya kazi kwa bidii kwa kuwatunuku vyeti pamoja na zawadi mbalimbali na si kusubiri kipindi cha sikukuu ya wafanyakazi, mei mosi lengo ni kuongeza ufanisi wa kazi.
Afisa utumishi na utawala Halmashauri hiyo Amandus Mtani, alisema baadhi ya watumishi wamekuwa wakifanya kazi kwa mazoea na huku wengine wakifanya kazi kwa kujituma.
Alisema kuwa kwa kutambua hilo Halmashauri imeanzisha utarabu maalumu wa kuwatambua wafanyakazi wake wanaojituma katika kutekeleza kuwahudumia wananchi na kuwatunuku vyeti pamoja fedha.
Afisa utumishi huyo alisema sambamba na hilo Halmashauri imeweka utaratibu wa kuwafikisha kwenye baraza la madiwani watumishi ambao wamekuwa wakitoroka kwenye vituo vya kazi na kusababisha kazi za serikali kukwama ili wajadiliwe.
Aliyasema hayo wakati akikabidhi vyeti na zawadi mbalimbali katika baraza la madiwani lililoketi katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.
Katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka 2019/20, halmashauri imetoa vyeti kwa wafanyakazi ambao ni watumishi na ambao si watumishi wa serikali wapatao kumi.
Aliwataja watumishi hao kuwa ni Magreth Kakoyo afisanyuki, Eva mkunda afisa Rasilimali watu ,Mariam Kimashi afisa maendeleo ya Jamii, Ibrahim Simbakavu dereva, Baraka Mazengo katibu wa vikao, Denis Mwapepe katibu wa vikao, na Saidi Rajabu Mhasibu Msaidizi.
Alisema licha ya hao waligawa vyeti na zawadi kwa wafanyakazi watatu ambao si watumishi ambao ni Omari Fundikira dereva,Pasko Msumeno mhudumu na John Fedha, mhudumu na kusema wote hao walikuwa wakifanya kazi kwa kujituma na kuonesha nidhaamu mahali pa kazi.
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Daudi Sichone ,alitumia fursa hiyo kuwataka watumishi kufaanya kazi kwa bidii ikiwa ni pamoja na kuepuka vitendo vya utoro wakati wa muda wa kazi.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.