Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoani Rukwa imewafikisha mbele ya mahakama ya wilaya ya Kalambo watu wawili akiwemo mkuu wa shule ya msingi Kipanga Tobias Masolo na mtendaji wa kijiji Nonadi Katito baada ya kupokea hongo ya shilingi laki tatu na ishirini kutoka kwa wazazi wa mwanafunzi aliyekuwa amepatiwa ujauzito na Justine Kandoro wote wakazi wa kijiji hicho.
Mkuu wa Takukuru mkoani humo Yustina Chagaka amesema viongozi hao kwa pamoja wamefikishwa mahakamani baada ya kula Rushwa kutoka kwa wazazi wa mwanafunzi wa darasa la sita shule ya msingi Kipanga mwenye umri wa miaka 16 aliekuwa amepatiwa ujauzito na kukatishwa masomo yake.
‘’Kesi mpya zilizofunguliwa mahakamani katika kipindi cha machi, 2021 ni nne hivyokufanya jumla ya kesi tisa zilizoendelea kusikilizwa mahakamani kwa kipindi hicho. Aidha katika kipindi hicho kesi moja ndio iliyotolewa uamuzi ambapo ilimtia hatiani mshitakiwa.’’ Alisema chagaka.
Aidha taasisi hiyo katika kipindi hicho imesaidia kusimamia marejesho ya fedha kwa wananchi waliotoa fedha zao kwa vyama vya ushirika vya mazao (AMCOS) pasipo kupewa pembejeo zao.
‘’ Kwa Halmashauri ya Kalambo takukuru tumesaidia kusimamia marejesho ya fedha shilingi 1,500,000/= kwa wananchi waliotoa fedha zao katika chama cha ushirika wa mazao cha Kanyere (Kanyere AMCOS) pasipo kupewa pembejeo. Alisema.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.