Wavuvi Wilayani Kalambo mkoani Rukwa wametakiwa kutumia fursa ya kufunguliwa kwa soko kuu la samaki la Kasanga Wilayani humokwaajili kuongeza vipato vyao na serikali kwa kuuza samaki na kuacha tabia ya kutumia njia za panya kupeleka samaki katika nchi jirani ya Zambia.
Wito unatolewa kwa wavuvi hao baada ya soko hilo lilojengwa kuanzia mwaka 2008 na kuwekewa jiwe la Msingin na aliyekuwa Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal mwaka 2012, huku likishindwa kufanya kazi kwasababu mbalimbali,ikiwapo kukosekana kwa miundombinu ya umeme na hata zana za kuhifadhia samaki, lakini hii leo limefunguliwa rasmi.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Msongela Palela alisema , wavuvi wote wa mwambao wa ziwa Tanganyika [upande wa Kalambo] hawana budi kuacha tabia ya kuuzia samaki majini na badala yake walete kwenye soko la samaki la Kasanga
‘’niwatake wavuvi wote kuleta samaki zenu hapa kwani miundo mbinu ya umeme, barafu na vichanja imeboreshwa, na wanunuzi wapo kwa wingi tofauti na hapo awali ambapo ilikuwa inawalazimu kupeleka samaki kwenye soko la Mpulungu nchini Zambia’’alisema msongela.
Afisa mifugo na uvuvi wilayani humo Wilbroad Kansapa alisema Licha ya kuzinduliwa soko hilo, bado baadhi ya wavuvi wanadaiwa kutumia njia za panya kununua samaki kwa wavuvi ndani ya Ziwa Tanganyika na sasa doria inahitajika ili kuhakikisha kuwa samaki zote zinaletwa .
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.